Jitambue, Ujitofautishe

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2022
Posts
289
Reaction score
489
Kila ukifika umri fulani na hadhi fulani unapaswa kubadilika pia kwenye mtindo wa maisha na hata watu wanaokuzunguka ikiwezekana pia wabadiliilishe kama unaona kabisa wanaweza kuleta shida kwenye maisha yako.

Mwaka 2015 Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete aliwahi kuulizwa je ni kipi alichokikumbuka na kukitamani akiwa madarakani kama Rais kwenye maisha yake.

Kikwete alisema ameyakumbuka maisha kabla hajawa Rais ambapo aliweza kukaa vijiweni kunywa kahawa na watu mbalimbali na kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwemo utani wa mpira wa miguu.

Mambo hayo yote akiwa madarakani aliyakosa kulingana na majukumu yake kama Rais pia mazingira kumtenga kulingana na cheo na hadhi yake ya kiuongozi.

Alimalizia kwa kusema anafurahi kwa sababu anamalizia kipindi cha uongozi wake kama Rais na kurudi kwenye maisha yake ya kawaida yenye uhuru.

Unapata picha kwamba kila jambo lina wakati wake kuna jua lakini kuna mvua, kuna huzuni na kuna furaha pia.

Hata kwenye maisha yako lazima ukubali mabadiliko kulingana na nafasi yako kwa wakati husika.
Ukiwa mhitimu wa kidato cha nne unapaswa kuonyesha utofauti Kati yako na yule wa darasa la saba.
Hivyo hivyo ukiwa msomi wa chuo kikuu na kadhalika unapaswa kuonekana hivyo pengine hata bila kuulizwa mtu akupime kwa fikra zako na matendo ya wazi.

Ukiwa mtu mzima ukiwa popote iwe kwenye jamii au mitandaoni uonekane kuwa mtu mzima usifananishwe na kizazi cha karne ya 21.

Usiwe mtu mzima mwenye kuonekana kila wakati kwenye udaku wa masuala ya ngono na uhuni ukitoa maoni mitandaoni, utadharaulika.

Usiwe mtu mzima wa kutoa maoni ya mihemko, chuki na dharau kinyume na uhalisia ulivyo mbele ya hadhara ya jamii. Utadharaulika.

Hata hivyo unapojitofautisha kulingana na umri wako na hadhi yako epuka kuonekana mbaguzi na mwenye dharau kwani matendo hayo hayaendani na kujitofautisha kunakozungumziwa.

Peter Mwaihola
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…