Jipu TANESCO Pwani Mkuranga

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,099
8,727
Jamani, naomba kama kuna mtu anaefanya kazi TAKUKURU, Mkuranga Pwani aniunganishe nae. Nataka nipate pesa za TAKUKURU nikakamue Jipu pale ofisi za TANESCO Pwani.

Huu ni mwezi wa tatu nimemaliza Jana, tangu nilipolipia kuunganishiwa umeme. Jamani kila nikipiga simu naambiwa tunakuja, nimekaa nyumbani miezi mitatu, nimeenda ofisini kwao mara kumi, kila nikienda wananiambia wanakuja. Nimepata tetesi kuwa ukijiongeza kidogo hao, wanajaa.

Niunganisheni na mtu yoyote wa TAKUKURU nitumbue jipu. Yaani ile timu ya kuunganisha umeme pale nasikia inanuka rushwa, 50,000 tu wanakuungia mi siwapi nataka niwatumbue.

Nisaidieni, nipo Kongowe mwisho.
 
Ni kwwli hakika nakumbuka tulitumia miez sita bila ya kuungiwa umeme mkuranga tanesko ni jipu hela mbele kama tai
 
Back
Top Bottom