Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,208
- 4,406
MAJIPU BUBU.
1) Kwenye msiba wa mamba chura samaki na wamo.
Wapo wakusoma namba,kambale changu na yumo.
Kimya kupiga jaramba,bubu haoni mvumo.
Yote ni majipu bubu,ngoja yaive uone
2) Jipu huliona jipu,waganga wanalijua
Japo kusema upupu,uoga kujilipua.
Subiri wale mapupu,jinsi watavyojilia.
Yote ni majipu bubu,ngoja yaive uone.
3) Kuni itatoa moshi,kipofu hawezi ona.
Japo ni kwa maandishi,figa yatajibizana.
Wafutahie waashi,kimya wakitulizana.
Yote ni majipu bubu,ngoja yaive uone.
5) Mengine yanajitamba,kwamba fahali wa shamba.
Ona uone ushamba,uwatazame magamba.
Hata kulicheza rumba,washindwa kwani jaramba
Yote ni majipu bubu,ngoja yaive uone.
6) Majipu ya lengelenge,yena yameota sugu.
Zidi ya banyamulenge,ni kama nazi za pugu.
Hayaponi kwa mlonge,hata kaa la tendegu.
Yote ni majipu bubu,ngoja yaive uone.
Shairi=JIPU BUBU.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160.