Jiondoe kwenye kifungo kisicho na ulazima

ibra87

R I P
Jul 22, 2015
5,614
5,347
Wasalaam wakuu,

Ni matumaini yangu kuwa kuna baadhi yetu tupo katika mahusiano. Mahusiano yenye mambo mengi kama kukera, kuliza na kuumiza.

Wengi walio katika mahusiano wamefika walipo wakipita katika mataizo mpaka kufikia hapa walipo. Mapito ya wengi waliopita ni mapito ambayo yaliwaacha na makovu moyoni, majonzi na vilio. Vilio vyao havikuonekana ni vyenye thamani lakini wakajaribu kusimama na hatimaye kufika hapa walipo. Lakini licha ya kupitia hayo na kuwafikisha hapa walipo hutakiwa kuendelea kuwa mtumwa... hutakiwi kuendelea kulia na kumshushia lawama Mungu.

Najua wengi mpo katika mahusiano ambayo yametawaliwa na chuki, usaliti, dharau na hata manyanyaso. Wengi mpo katika muhisiano ambayo kamwe hakuna faraja wala upendo wa dhati. wanawake wanaishia kupigwa, kudhalilishwa na kufanyiwa vitendo ambavyo huwezi kuvisema hadharani.

Lakini licha ya kufanyiwa hayo yote bado wametulia, bado wanateseka ndani kwa ndani, bado wanavumilia na kuamini ipo sikuwataishi katika amani na utulivu. wapo wanaoletewa wanawake majumbani lakini bado waliendelea kuvumilia. Wapo wanaume wanaonyanyaswa na kunyimwa unyumba, wapo wanaume wanaofanywa mazezeta na wake zao majumbani mwao lakini still wanavumilia. Hivi utaishi katika hili mpaka lini? Utaishi katika kifungo hiki mpaka lini?

Tuseme bila uliyenae huwezi kuishi? Kwanini unalikubali hili ndani ya moyo? Simama wewe kama wewe huku ukijiamini kuwa unaweza. Kuanza moja sio ujinga. Piga hatua na songa mbele hili litakufanya utoke ndani ya kifungo kisicho cha lazima

Ahsanteni sana

Ibra87
 
Yan af cjui nimemfanyia nn mana km kumuheshim nimemuheshimu sana ila nimenyosha mikono.jaman aaahaaa
huwezi na hutoweza mrizisha binadamu yoyote yule!binadamu huwa tuna tabia ya kutaka kutimiziwa shida zan,na shida inapoisha huitaji kutimiziwa zingine!cha muhimu kwako chaweza kuwa cha kawaida kwa mwingine...usipaniki
 
Ni kweli mkuu lakini wengine amejikuta wakiwa katika wakati mgumu kutokana na hili
ukomavu wa kisaikolojia ni wa taratibu kama ulivyo ukuaji wa kimwili!utatambaa,uta simama dede,utatembea na mwishowe utakimbia na hata kuruka!ndivyo ilivyo ukuaji wa kisaikolojia,utaumizwa hapa,halafu nawe utamumwiza yule,utalia kutengwa na mpenzi,au kuchukiwa na umpendaye,na muda mwingi kwa utoto wa kiakili yanapo tokea matatizo ya kimapenzi unahisi we ndiye mkosefu,mwenye madhaifu na usiye faa...kumbe wakati mwingine mpenzio ndio mwenye shida...kukomaa kiakili na kisha kisaikolojia kunataka muda,jipe moyo utayashinda
 
Nitafuata ushauri wako soon kwakweli, japo kuwa single ngumu sana
jiondoe katika hilo.. Usiishi kwa kumtegemea mtu na kusema bila yeye huwezi... Ipo siku ataondoka je ni vp utaishi?
 
Mule muleee wale wooote wanaokua wanaomba ushauri wapite hapa
 
Back
Top Bottom