Je ukitaka ziingie kwny gallery zile ambazo tayari zipo whatsapp unafanyaje?
Hapo unaweza kutumia njia zingine ya kuangali nakudownload picha au video ambazo unahitaji zionekane katika gallery.
unaweza kuchagua na kutumia njia hizi tatu;-
- kuzuia moja kwa moja picha na video zisijidownload kabisa.
- Kuzuia picha na videos zisijidownload kwa baadhi ya watu au magroup.
- Kuruhusu picha na videos zijidownload kwa baadhi ya watu au magroup.
kuzuia moja kwa moja picha na video zisijidownload kabisa.
Katika whatsapp kuna kipengele kimewekwa kwajili ya kuzuia au kuamua media zipi unaweza kusave moja kwa moja katika simu yako. Hapa nitakuonyesha namna ya kuzuia media zote zisiweze kujidownload ata kama utakuwa umewasha data. Utakapo ingia katika whatsapp yako basi wewe mwenyewe utaamua picha au video zipi uweze kuzidownload. Hakuna haja ya kutumia MB nyingi kwa vitu ambavyo havina maana. Fuata hatua zifuatazo:-
1. Ingia katika whatsapp yako.
2. Bonyeza alama ya vidoti vitatu upande wa kulia juu.
3. Nenda katika
settings.
4.Bonyeza
Data and Storage Usage.
5. kwenye kipengele cha MEDIA AUTO-DOWNLOAD bonyeza sehemu imeandikwa
When using mobile data.
6. Ondoa alama ya vema katika kila kiboksi.
6. Bonyeza OK na hapo utakuwa umemaliza.
Kuruhusu picha na videos zijidownload kwa baadhi ya watu au magroup.
Ni kitu kizuri kuruhusu picha na video zijidownload kwa baadhi ya watu muhimu kama vile picha za familia, jamaa wa karibu, ndugu n.k. Fuata hatua zifuatazo:-
1. Ingia katika whatsapp yako.
2. hakikisha kwanza unafuata hatua zote hapo juu za
kuzuia moja kwa moja picha na videos zisijidownload kabisa.
3. Chagua namba au Chat yoyote ambayo ungependa media ziweze kujidownload moja kwa moja.
4.Ingia katika profile yake(DP).
5. Chini bonyeza
Media auto-download.
6. Weka alama ya vema katika kipengele kilichoandikwa
Enable custom media auto-download.
7.Weka alama ya vema katika vipengele vyote vilivyo baki.
8. Mwisho.
Kuzuia picha na videos zisijidownload kwa baadhi ya watu au magroup.
Kuna baadhi ya watu au magroup usingependa kudownload videos au picha. Fuata hatua hizi:-
1. Ingia katika whatsapp yako.
2. Fuata hatua 1 – 6 zilizopo hapo juu za
Kuruhusu picha na videos zijidownload kwa baadhi ya watu.
3. Ondoa alama ya vema katika vipengele vyote vya chini.
Kama haujaelewa basi unaweza ukasoma zaidi hapa https://tztechforums.com/community/...deos-zisiji-sownload-katika-whatsapp/#post-56