Jinsi ya kuzuia picha na videos za WhaatsApp zisionekane katika gallery ya simu yako

Kazinza26

Member
Apr 15, 2019
9
18
Unaweza ukawa na watu kibao au magroup mengi katika whatsapp ambayo yanaweza kuleta usumbufu kutokana na picha au video zinazo tumwa.
Kama hauhitaji usumbufu huo na husingependa picha au video hizo zionekane katika gallery ya simu yako basi fanya na kufuata hatua fupi zifuatazo:-
  1. Ingia katika whatsapp yako.
  2. Nenda katika settings.
  3. Bonyeza chats.
  4. Ondoa alama ya vema katika sehemu iliyoandikwa show media in gallery
  5. Hapo utakuwa umemaliza.
Unaweza ukasoma zaidi hapa https://tztechforums.com/community/...sapp-zisionekane-katika-gallery-ya-simu-yako/
 
Je ukitaka ziingie kwny gallery zile ambazo tayari zipo whatsapp unafanyaje?
Unaweza ukawa na watu kibao au magroup mengi katika whatsapp ambayo yanaweza kuleta usumbufu kutokana na picha au video zinazo tumwa.
Kama hauhitaji usumbufu huo na husingependa picha au video hizo zionekane katika gallery ya simu yako basi fanya na kufuata hatua fupi zifuatazo:-
  1. Ingia katika whatsapp yako.
  2. Nenda katika settings.
  3. Bonyeza chats.
  4. Ondoa alama ya vema katika sehemu iliyoandikwa show media in gallery
  5. Hapo utakuwa umemaliza.
Unaweza ukasoma zaidi hapa https://tztechforums.com/community/...sapp-zisionekane-katika-gallery-ya-simu-yako/
 
Mm suali langu ni kuwa unaweza kuzifanya zisionekane kwenye gallarry, ila zikawemo kwenye file au ndio pia hazitakuepo kwenye file?
 
Je ukitaka ziingie kwny gallery zile ambazo tayari zipo whatsapp unafanyaje?
Hapo unaweza kutumia njia zingine ya kuangali nakudownload picha au video ambazo unahitaji zionekane katika gallery.
unaweza kuchagua na kutumia njia hizi tatu;-
  1. kuzuia moja kwa moja picha na video zisijidownload kabisa.
  2. Kuzuia picha na videos zisijidownload kwa baadhi ya watu au magroup.
  3. Kuruhusu picha na videos zijidownload kwa baadhi ya watu au magroup.

kuzuia moja kwa moja picha na video zisijidownload kabisa.
Katika whatsapp kuna kipengele kimewekwa kwajili ya kuzuia au kuamua media zipi unaweza kusave moja kwa moja katika simu yako. Hapa nitakuonyesha namna ya kuzuia media zote zisiweze kujidownload ata kama utakuwa umewasha data. Utakapo ingia katika whatsapp yako basi wewe mwenyewe utaamua picha au video zipi uweze kuzidownload. Hakuna haja ya kutumia MB nyingi kwa vitu ambavyo havina maana. Fuata hatua zifuatazo:-
1. Ingia katika whatsapp yako.
2. Bonyeza alama ya vidoti vitatu upande wa kulia juu.
3. Nenda katika settings.
4.Bonyeza Data and Storage Usage.
5. kwenye kipengele cha MEDIA AUTO-DOWNLOAD bonyeza sehemu imeandikwa When using mobile data.
6. Ondoa alama ya vema katika kila kiboksi.
6. Bonyeza OK na hapo utakuwa umemaliza.

Kuruhusu picha na videos zijidownload kwa baadhi ya watu au magroup.
Ni kitu kizuri kuruhusu picha na video zijidownload kwa baadhi ya watu muhimu kama vile picha za familia, jamaa wa karibu, ndugu n.k. Fuata hatua zifuatazo:-
1. Ingia katika whatsapp yako.
2. hakikisha kwanza unafuata hatua zote hapo juu za kuzuia moja kwa moja picha na videos zisijidownload kabisa.
3.
Chagua namba au Chat yoyote ambayo ungependa media ziweze kujidownload moja kwa moja.
4.Ingia katika profile yake(DP).
5. Chini bonyeza Media auto-download.
6. Weka alama ya vema katika kipengele kilichoandikwa Enable custom media auto-download.
7.Weka alama ya vema katika vipengele vyote vilivyo baki.
8. Mwisho.

Kuzuia picha na videos zisijidownload kwa baadhi ya watu au magroup.
Kuna baadhi ya watu au magroup usingependa kudownload videos au picha. Fuata hatua hizi:-
1. Ingia katika whatsapp yako.
2. Fuata hatua 1 – 6 zilizopo hapo juu za Kuruhusu picha na videos zijidownload kwa baadhi ya watu.
3.
Ondoa alama ya vema katika vipengele vyote vya chini.

Kama haujaelewa basi unaweza ukasoma zaidi hapa https://tztechforums.com/community/...deos-zisiji-sownload-katika-whatsapp/#post-56
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom