Jinsi ya kuwa jasusi wa kujitegemea; Na itakavyokusaidia katika Maisha yako ya kila Siku hasa kiuchumi na kijamii

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,050
Reaction score
79,392
JINSI YA KUWA JASUSI WA KUJITEGEMEA; NA ITAKAVYOKUSAIDIA KATIKA MAISHA YAKO YA KILA SIKU HASA KIUCHUMI NA KIJAMII.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Nianze kwa kusema mimi sio jasusi, sijawahi kusomea ujasusi, sipo katika mazingira ya ujasusi. Wala sina ukaribu na watu WA aina hiyo.

Mimi ni mwandishi na mtunzi. Kama mjuavyo Mtunzi ni package inayobeba packages nyingi. Watunzi hatuko limited, mawazo yetu yanapaa zaidi ya upeo WA macho. Sehemu ambako milango ya fahamu ya kawaida haifiki basi huko ndiko makao yetu.

Ukituita much know wala sio tatizo. Na hiyo ni moja ya sifa kuu ya mtunzi mahiri.

Sasa basi, kutokana na baadhi ya watu kuwasiliana na mimi, wengi wao wakidhani huenda mimi ni Jasusi, wakitaka ati kama kuna upenyo niwapenyeze huko🙂 , ili wawe maafisa vipenyo square. Wengine mtaani nikiwaona wanatamani KAZI hiyo

Nikasema acha nitumie uelewa wangu, Akili ya utunzi, falsafa, saikolojia, sosholojia kuwasaidia kwa nafasi yangu.

Kwanza, elewa KAZI ya ujasusi sio kazi ya kuitamani, sio KAZI ya kutaka sifa, kama lengo lako la maisha ni kuwa na furaha, na kupewa heshima.
Elewa, kwa kiasi kikubwa KAZI hiyo inalenga kuwatumikia Wakubwa, kikundi Fulani, na sio kuitumikia Jamii na tabaka la chini.
Kwa nje utawatumikia tabaka la chini ikiwa kuna maslahi ya wakubwa.
Kazi ya ujasusi itakuwia ngumu zaidi ikiwa viongozi waliojuu yako ni Waovu, wahalifu, na wasio na roho ya utu wakati wewe huenda ni muadilifu, mchamungu n.k
Hivyo utaifanya kwa maumivu, majuto, na hutoipenda. Zaidi utaishia kujiingiza katika mitindo ya maisha hatarishi, kama unywaji wa pombe kupitiliza, kutumia madawa Fulani ya kulevya ili kuilaghai akili yako ujione upo sawa.

Hata hivyo niliwahi kuandika kuwa, watu hukuchukulia vile ulivyo, vile utakavyojionyesha, kulingana na msimamo wako.
Hivyo kama ni muadilifu na unaroho safi, jitahidi siku za mwanzoni uonyeshe hivyo, usiwe mwoga kwa kuogopa kukosa nafasi.
Ishi na penda uadilifu. Watu wakujue hivyo.

Hii itakusaidia kama utaingia kwenye ujasusi upewe mission ambazo zinauadilifu au mfanano wa uadilifu. Hutapewa kazi za hatari za kihalifu na dhulma.
Na ukipewa unauwezo wa kukataa, ingawaje kuna Kiapo.

Ooh! TaikonMaster mbona maneno mengi. Unatuchosha!

Anyway! Twende kwenye mada sasa.

Mambo yafuatayo yatakufanya uwe Jasusi wa kujitegemea, ambapo itakusaidia katika mishemishe zako za kila siku, iwe ni mahusiano, si unasikia watu wanalia kuhusu mahusiano? Hutakuwa mmoja wao.
Iwe ni kazini au masuala ya kifedha na kiuchumi. Husikii vijana wakillamika hakuna ajira, sijui mshahara mdogo, sijui serikali, ukiwa jasusi huwezi kulalamika kwa sababu unaona mlango wa kila tatizo ulipo.

Twende KAZI;

Jinsi ya kuwa jasusi wa kujitegemea; Na itakavyokusaidia katika Maisha yako ya kila Siku hasa kiuchumi na kijamii;

1. Jifunze uchambuzi wa Kisaikolojia na Tabia za Binadamu(Psychological Profiling & Human Behavior Analysis).

Kwa waliosoma kozi zinazohusu muingiliano na mahusiano ya watu kama Ualimu, uanasheria, Udaktari, upolisi, ujasusi n.k. Lazima wasome kozi ya Saikolojia.
Saikolojia ni moja ya kozi muhimu na applicable katika maisha yako ya kila siku.
Sasa ili uwe jasusi wa kujitegemea lazima ujue basic au ukiweza Kwa kiwango cha juu saikolojia kama

a) Kusoma lugha ya mwili (body language)

b) Kugundua uongo na nia zilizofichika Kwa kuangalia body language, sauti ya mtu, n.k.

c) Kuelewa tabia ya mtu kabla ya kumuamini au kushirikiana naye

Faida: Unajikinga na usaliti, udanganyifu na uharibifu wa kihisia au kifedha.

2. Jifunze, Uelewa wa Mazingira na Tathmini ya Hatari (Situational Awareness & Risk Assessment)
Sasa unajua saikolojia ya watu wanaokuzunguka. Yaani akili, hisia, tabia, mitazamo, n.k. usiishie hapo unaishi kwenye mazingira.
Mazingira ni kila kitu kinachokuzunguka hii ulisoma shule.
Mazingira ya asili na mazingira yaliyobuniwa na bin adamu.
Kila kitu unachokiona kwenye mazingira yako kina maana na sababu yake.
Kwenye mazingira kuna vitu(asili na man made), majira na wakati, Hali ya hewa, ukanda, n.k.

Ni muhimu kujua mazingira yako popote ulipo;

a) Kugundua vitu visivyo kawaida katika mazingira yako.
Utajuaje kitu sio cha kawaida?
Kila kitu kinamazingira yake, hilo linafahamika. Kitu kisipokuwa sehemu yake ni ishara ya Kwanza kukujulisha kuwa kuna Jambo halijakaa sawa.
Mfano, kumkuta Kuku Mbugani. Hiyo sio kawaida.

Pia kitu kisipofuata mtiririko au mpangilio uliozoeleka wawakaida.
Kila Jambo linamkondo wake.
Mfano,
ukuaji wa mtoto. Mtoto akifikisha miaka miwili anatakiwa awe amesimama na kutembea mwenyewe. Sasa ukiona atembei hiyo sio kawaida.

Kwenye biashara, umemweka mfanyakazi kila wiki anakuletea hesabu ya laki mbili labda lakini ghafla apunguze alete laki moja au iongezeke laki 4.

b) Kutambua watu au hali zenye hatari mapema.
Sasa kunakutambua mazingira, watu, Hali na ishara zisizo za kawaida.

Faida: Unapunguza hatari ya kuingia mikataba mibaya, mahusiano hatarishi au kupoteza fedha

3. Jifunze Uhandisi wa Kijamii na Mbinu za Ushawishi (Social Engineering & Influence Tactics)
Uhandisi)
Uhandisi jamii ni njia ya kisasa ya kitumia maarifa na ujuzi wa kiuhandishi kubuni na kutatua matatizo yako na jamii kwaajili ya maendeleo. Wakati wahandisi wakibuni na wakijenga miundombinu na madaraja na majengo wewe mhandisi jami jukumu lako litakuwa kubuni na kujenga ushawishi, fikra, wazo, mipango katika jamii inayokuzunguka.

Kwa ufupi hapa;
a) kujifunza jinsi ya kuwashawishi watu kwa ustadi.
Hii itakusaidia kujenga Network nzuri, kukuza jina ma biashara yako, kupata promo kazini n.k.

b) Kuelewa namna watu wanavyoweza kukutumia au kukuathiri kisaikolojia.
Maisha ni kuwatumia wengine, kujitumia, kutumiwa au kutumiana.
Jenga mutual relationship (mutualism) wanasiasa na wanauchumi hupendelea kuita Win- Win relationship. Hii nawaambiaga hata kwenye familia, mahusiano, epuka kuingia kwenye mahusiano na mwanamke asiye na mchango wowote kiuchumi. Hiyo kiintelejensia haijakaa sawa. Hakuna usalama. Hapo. Hiyo inaitwa parasitism, yaani unanyonywa na kupe wakati wewe hufaidiki kitu. Asijekukuambia amekuzalia. Elewa watoto mliozaa ni wake pia.

Hii itakusaidia kwenye final ambush au final touch.

Faida: Unaweza kuuza wazo au bidhaa kwa ufanisi, kujenga mitandao bora ya kijamii/kibiashara

4. Jifunze, jasusi Kutoka Taarifa za Wazi Mtandaoni
(Open Source Intelligence (OSINT)
Tumia mitandao ya kijamii kwa faida, kama sehemu ya kupata habari na kujifunza. Lakini lazima ujue usahihi wa habari na mafunzo unayoyapata huko.
Unaweza kuacha taarifa zako kimkakati kama ni sehemu ya KAZI yako na haigusi faragha yako.
Siku hizi mambo mengi yapo mtandaoni. Na kila mtu anaweza kuwa jasusi akitaka. Kwani msingi mkuu wa ujasusi ni kuwa na taarifa, hata hivyo kuzichakata, kuchanganua, kuzihifadhi na kuzitumia pia ni Jambo muhimu.

Haya;
a) Kutafuta taarifa halali na sahihi kwa kutumia Google, mitandao ya kijamii n.k.

b) Kuchunguza historia ya mtu, kampuni, au mazingira kabla ya kufanya uamuzi.
Sio rahisi kutapeliwa kama utakuwa makini kwenye eneo hili kwa habari za mitandao.
Kampuni imekuja inataka kitu kutoka kwako ifuatilie mtandaoni.
Tumia kanuni mbalimbali za kukufanya uwe salama

Faida: Unajilinda dhidi ya udanganyifu, utapeli na upotevu wa muda/pesa

5. Jifunze kupanga Mipango ya Kiutendaji na Uamuzi Katika Shinikizo ( Operational Planning & Decision Making Under Pressure)
Huwezi kufikia shabaha na malengo yako kama hujui kupanga mipango na huna mipango. Mipango ya kiutendaji ni lazima ujifunze kuipanga na kuchukua maamuzi sahihi ya kuitekeleza hata katika shinikizo.
Katika mafunzo ya kulenga shabaha. Utafundishwa kulenga shabaha, kisha utafundishwa kulenga shabaha ukiwa under pressure.
Yaani kutimiza malengo licha ya kukabiliwa na changamoto zingine maisha.
Jifunze kufanya maamuzi sahihi, ambayo hutokana na uchaguzi sahihi, mbinu sahihi na wakati sahihi.

Haya;
a) Kupanga mikakati ya maisha, biashara au miradi

c) Kujifunza kufanya maamuzi bora hata ukiwa katika hali ya presha

Faida: Unakuwa na uwezo wa kusimama imara, kutatua matatizo na kufanikisha mipango

6. Jifunze kujenga na Kubadili Utambulisho, Faragha na Usalama Mtandaoni (Disguise, Privacy & Digital Security)
Haya ni mambo muhimu kuzingatia;

a) Kulinda taarifa zako binafsi kama nywila, akaunti, picha na mawasiliano.
Sio lazima kupost taarifa zako za msingi mitandaoni kama sio sehemu ya KAZI yako. Yaani haikuongezei chochote kwenye malengo yako.

b) Kuepuka kufuatiliwa au kudhuriwa kupitia mitandao.
Kudukuliwa, watu kukufanyia Bullying, kujua hatua zako, inaweza kukudhuru kiakili na kihisia.

Faida: Unajilinda dhidi ya watu wenye nia mbaya, utapeli wa kimtandao, na kuingiliwa kwa maisha yako binafsi

7. Jifunze Ufuatiliaji wa kijasusi na Mbinu za Kujikinga na kufuatiliwa. (Surveillance & Counter-Surveillance Basics).
Lazima ujue mtandaoni sio sehemu ya siri kwamba ni chumbani kwako.
Hata uwe IT vipi lazima uwe na tahadhari na usijiachie kama upo ndani ya kaburi lako mwenyewe.
Jifunze kujua matapeli wa kimfumo, kudukuliwa na kujua basics za udukuzi,
Kwenye maisha ya kawaida, jihami, elewa Kuta zinamacho. Jifunze kujikinga na wafuatiliaji wa siri na mipango yako. Usiweke wazi mipango yako kwa watu au mtu yeyote kabla mipango hiyo haijatimia.

Haya;
a) Kugundua kama unaangaliwa au unachunguzwa (mtandaoni au maisha ya kawaida)

b) Kutambua dalili za mtu anayekutega au anayetaka kukudhuru

Faida: Unajilinda wewe, familia yako, biashara zako, na heshima yako dhidi ya watu wenye madhara

Kufikia hapa nimechoka na sina la ziada.

Acha nipumzike, makande time!

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mada nzuri ila ukweli ni kwamba kam wewe sio jasusi basi unatumika na majasusi wa kimfumo.

Ni nadra sana ukakuta mtu mwenye ushawishi na network akakosa kutumika kwenye mambo hayo hata Kwa wakati Fulani Kwa malengo Fulani iwe Kwa kujua au kutokujua.

Jambo la msingi kabisa kwenye mada Yako ni
-Kutengeneza network na ushawisi kwa maslahi Yako
-Kujilinda na kuepuka hatari
-Kuishi Kwa machale machale
-Somo la saikolojia ya binadamu ni muhimu sana japo basics
 
-Kutengeneza network kwa maslahi Yako
-Kujilinda na kuepuka hatari
-Kuishi Kwa machale machale

Upo sahihi Kabisa.

Kuwa na ushawishi kunafanya rada za majasusi kukumulika,
Kutaka kukujua
Kisha kuona watafaidika nini na wewe katika shughuli zao
 
Binafsi hizo kazi sizipendi hata kidogo ila Ukiwa tuu na kaushawishi Fulani huwezi Wakosa Kwa Ajili ya faida zao.

Huwa nawashangaa wanaozipenda maana ni kazi zinakunyima uhuru Fulani na unatumikia wakubwa.

Kitu nimejifunza hapa ni kwamba Bora uoneshe character zako za utu mapema Ili usije ingia au ingizwa kwenye mission za ukatili Kwa manufaa y Wanasiasa 😆😆

Hela Haina maana Kwa mpenda Haki na kujali utu.
 
Binafsi hizo kazi sizipendi hata kidogo ila Ukiwa tuu na kaushawishi Fulani huwezi Wakiwa Kwa Ajili ya faida zao.

Huwa nawashangaa wanaozipenda maana ni kazi zinakunyima uhuru Fulani na unatumikia wakubwa.

Kitu nimejifunza hapa ni kwamba Bora uoneshe character zako za utu mapema Ili usije ingia au ingizwa kwenye mission za ukatili Kwa manufaa y Wanasiasa 😆😆

Hela Haina maana Kwa mpenda Haki na kujali utu.

Kweli Kabisa

Alafu wakubwa wenyewe mwishoni huwaga wanakuambia wewe ndio ulitaka KAZI hizo na tulikulipa,

Na kweli wanalipwa ikiwezekana wanaulizwa mission inatagharimu kiasi gani pamoja na malipo yao.

Kama ungekuwa muadilifu usingetumwa KAZI chafu.

Wanaokuteua hawakurupuki, lazima kuwe na vikao na cv za maafisa zichambuliwe.
 
Tunasonga mbele maisha yaendelee kazi na utu 🤣🤣
 
Hayo mambo yote mtu hafundishwi bali anazaliwa nayo ukiona mtu anafundishwa na kweli akaiva kaa ukijua mtu huyo alikua anakumbushwa tu juu ya uwezo uliojificha ndani yake
 
WORKING FOR KILLERS IS A SURE WAY OF BOOKING THE PLACE IN HELL!
 
Kuna kujifunza na kufundishwa.
Hakuna anayezaliwa anajua ni aidha ujifunze au ufundishwe
Nakupa mfano mdogo....kila mtu ambaye anaweza kuongea basi kwa asili mtu huyo anaweza kuongea lugha yoyote ile duniani ila kwa wale ambao hawana uwezo wa kuongea hata uwafundishaje hawezi kuongea.

Ujasusi unazaliwa nao na wapo watu hawajazaliwa kuwa majasusi hivyo hata uwakate mitama hawezi kuwa hivyo
 
Back
Top Bottom