Jinsi ya Kutengeneza Pesa Kutumia Canva kama tool ya graphics design

Jinsi ya Kutengeneza Pesa Kutumia Canva kama tool ya graphics design

FestoKaguo

Senior Member
Joined
Apr 1, 2022
Posts
128
Reaction score
202
Soma usije kulaumu mtu baadae haya maelezo ni zaidi ya kuwa na degree
Watu wengi wanaotumia Canva huwa wanatumia kutengeneza posters za social media kama za Instagram, facebook, twitter n.k, lakini JE unajua unaweza kuitumia Canva hiyo hiyo kutengeneza pesa zaidi out of hizo social media posters?

Najua huenda ulikuwa haufahamu kwahiyo sasa
hapa naenda kukueleza njia mbali mbali unazoweza kuzitumia ili kuifanya Canva iwe chanzo chako cha kipato na inaweza kukupa hela ya bando kama sio ya kodi na kula, na uzuri wa Canva haikuhitaji uwe na ujuzi mkubwa wa graphic design kama hawa watumiaji wa Adobe softwares.

Naenda kukuandikia njia tano zinazoweza kukuletea kipato kwa kutumia Canva:
20250317_200826.jpg

Njia ya kwanza kabisa ni Kuuza Templates za Canva ulizozidesign.

Wafanya Biashara wengi na content creators wa social media wanahitaji sana templates za haraka kwa ajili ya kupost kwenye social media kama
✅ Instagram
✅️TikTok
✅ YouTube
✅️Facebook
✅️Youtube
20250317_201707.jpg

Sasa ukiwa unaweza kutumia Canva inakuwa rahisi wewe kudesign hizo templates na kuziuza kwa wafanyabiadhara au majukwaa ya mtandaonikama Etsy ambayo unaweza kujisajili hapa ( bit.ly/43fdnU6), Creative Market, na Gumroad ( haya ni majukwaa unayoweza kuyatumia kuuza hizo designs zako)

Kitu cha pili unaweza kuitumia Canva kwa ajili ya Kufanya kazi kama Freelance Graphic Design ( Graphics designer)

Kumbuka ukiwa na Canva, unaweza kutoa huduma kama:
✅ Kutengeneza logo za biashara ndogo ndogo
✅ Kudesign social media posters
✅Kudesign Flyers na brochures
✅️ Kudesign presentation designs kwa ajili ya kampuni na walimu n.k

Kazi zote hizo unaweza kutafuta wateja kwenye freelancing platforms kama Fiverr, Upwork, na Facebook Groups za biashara mbalimbali ukawauzia watu.

Njia ya tatu unaweza kutumia Canva kuunda Digital Products na ukaziuza
Hapa unaweza ukadesign au kutengeneza
✅ E-books na workbooks kwa ajili ya wanafunzi na walimu
✅ Unaweza kutengeneza planners na journals za productivity

Na hizi products unaweza kuziuza kwenye Etsy, Gumroad, au Shopify.
20250317_202310.jpg


Njia nyingine Canva inaweza kukusaidia kutengeneza na Kuuza Print-on-Demand Products kama T-shirts, stickers, Posters, Wall arts n.k, Canva inaweza fanya.

Unaweza upload hizo designs zako kwenye Redbubble, Teespring, na Printify, na upate pesa kila mtu anaponunua bidhaa yako.

Bonus Tip: Canva Affiliate Program!
Ukiwa na Canva pro utaweza kutumia hizo features zote pasipo kuwa limited kwenye vitu vya kutumia, ukitumia free Canva mara nyingi templates unazopewa zinakuwa limited na haziwi na ubora mkubwa kuliko zile za Canva pro.

Ukihitaji Canva pro unaweza kunicheki whatsapp kwa namba wa.me/255765772976 plus utapata na kozi ya Canva free kabisa kwa Lugha ya kiswahili incase haujui kabisa kutumia Canva.


20250317_203812.jpg

Tuendelee na njia namba tano sasa Canva inaweza kukusaidia kufundisha watu ambao hawajui namna ya kuitumia na kujiingizia kipato kizuri tu. Unaweza kufundisha watu wengine jinsi ya kutumia Canva kwa njia zifuatazo:
1. Moja unaweza Kufungua YouTube channel na kutoa tutorials mbali mbali za jinsi ya kutumia Canva

2. unaweza Kuuza kozi zako kwenye majukwaa ya kufundishia kama Udemy, skillshare na Teachable
Na njia ya tatu unaweza kutoa huduma za coaching kwa watu wanaotaka kujifunza Canva.

Kama umependa thread ingia chimbo kula pindi usisahau kunicheki wa.me/255765772976 nikupe CANVA PRO
 
Back
Top Bottom