Jinsi ya kutengeneza kashata za ufuta

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,103
Mahitaji
Ufuta kg2
Sukari 1/2

Jinsi ya kutengeneza

Chukua ufuta peta na toa takataka zote

Kisha tia ndani ya sufuria weka maji osha na chekecha michanga kama unavyo chekecha mchele kutoa mchanga kisha chuja maji na uanike juani ukikauka uukaange kidogo mpaka unukie na kuwa brown kisha chukua sufuria weka sukari na ubandike jikoni.

Kisha koroga mpaka sukari ilainike na uweke ufuta wako kisha geuza geuza mpaka ichanganyike na ishikane, ipua ufuta harakaharaka na uweke katika kibao cha kusukumia chapati au meza.

Chukua kisukumio paka mafuta sukuma litokee duara kama chapati, chukua kisu kikali kata muundo wa pembe nne au upendavyo na uache ukauke ukikauka utoe na uhifadhi tayari kwa kuliwa, ukitaka Kufanya madonge ukishautoa tu jikoni nawa mikono yako anza kuviringisha vitonge huku ukiwa unauchovya mkono wako kwenye mafuta au maji kidogo ili sukari isinase mikononi.

Na kashata za karanga unafuata maelekezo kama haya isipokua kashata za karanga unaweza tumia unga wa karanga au karanga zilizochubuliwa maganda nakusafishwa.


1645520161559.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom