Jinsi ya kutengeneza bootable flash bila kutumia software yoyote

Jinsi ya kutengeneza bootable flash bila kutumia software yoyote

Omaryjr1

Member
Joined
Jun 8, 2017
Posts
17
Reaction score
26
JINSI YA KUTENGENEZA BOOTABLE FLASH BILA KUTUMIA SOFTWARE YOYOTE*
mwanakwetu habari. Leo nimeona nishare nawe somo hili dogo but naamini litakuwa na nanufaa makubwa kwako na kwa wengine, baada ya hili somo usisahau kushare na wengine.

Kabla ya kuanza somo hili niseme mambo mawili.

1. Kama unataka trick mbalimbali za computer kwa njia ya video basi tembelea website yangu mjuzishule.tech

2. Kama unatamani kujua computer kiundani jiunge na online class ambalo ni darasa linalofundisha masomo mbalimbali ya computer kwa njia ya video hatua kwa hatua na hauhitaj kuwa online muda wote kujiunga, pia hakuna kuchelewa wala kuwahi hapa, Lengo ni kuandaa watu wenye uwezo wa kuelewa sio kukariri ili waweze kujiajiri.
(garama na muda wa kumaliza hutofautiana kulingana na somo husika)

Hapa kuna masomo kama jinsi ya kutengeneza blog, HTML& CSS(Website development), graphics & designing, PHP, JAVA, microsoft office, database na mengine.
Ukihitaji kujiunga wasiliana nami kwa email *obbymjuzi@gmail.com*
*tuendeleee....*

Tunaposema bootable flash hii ni flash itakayokuwezesha kuweka windows mpya kwenye computer yako kwa kutumia flash badala ya CD.

Hii inaweza kukusaidia kuweka windows kwenye computer ambayo haina mlango wa CD au mlango wake umeharibika.

Technology inakuwa kwa kasi sana hivyo ni muhm sana kujifunza mambo haya ili tusibaki nyuma. Kumbuka bootable flash inaweza kufanya kaz kama flash nyingine yaani kuamisha vtu kubeba vitu n.k. kwahiyo haimaanishi kwamba flash hii inakuwa imekufa.
Njia hii hutumika pia kuformat flash au memory inayogoma kuformatiwa.
kwa kufata hatua hizi chache utaweza kufanya hivyo.

1. a) Nenda kwenye sehem ya kusearch andika cmd then utaiona, right click na chagua run as administrator

b) au bonyeza windows button na R then andika CMD then ENTER

2. Kitatokea kipage cheusi chenye maandishi meupe, andika DISKPART then ENTER

3. andika LIST DISK then ENTER

4. Zitakuja disk nyingi na majina yake mfano (removable disk) au disk 1.
Chagua disk ya flash yako kwa kuandika
Mfano SELECT DISK 1 then ENTER( ni vema kuangalia herufi ya flash yako kwenye my computer kabla hujachagua)

5.andika CLEAN then ENTER

6. Ikimaliza andika CREATE PARTITION PRIMARY then ENTER

7. Andika SELECT PARTITION 1 then ENTER

8. andika FORMAT FS=NTFS QUICK

9. iache iformat ikimaliza andika ACTIVE then ENTER

10. Andika assign then ENTER,

11. hapo utakuwa umemaliza, andika EXIT hicho kipage kitapotea na flash yako itakuwa imekuwa bootable, unaweza kuchukua mafile ya windows na kuyaweka humo na yakafanya kazi kama vile unavyotumia CD.

Kumbuka unapotaka kuweka windows usichanganye mafile ya windows na vitu vingine mfano nyimbo au vdeos, ni muhim flash ikawa na windows tu, ukimaliza kuweka windows unaweza kuiondoa windows na kuweka mambo unayoyataka.
>>>>Asante<<<
 
Kaka mbona kwangu inagoma inaniandikia THERE IS NO VOLUME SELECTED hii ni memory card lakini

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujaselect volume ambayo unataka itumike muda huo. Angalia memory yako imesoma drive letter gan kisha ukija hapo angalia iko volume gani kisha select kwa kuandika select volume x(hapa x weka nmba ya volume)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ebwana mimi naomba unifundishe kitu kimoja. Nawezaje ku restore files ambazo nimeshazifuta mpaka kwenye recycle bin?
 
Nimependa mnoo,nakupataj mkuu nijifunze physically?
Habar za online haziko efficient kihivyo kama nijuavyo

thA God thA bubbs!!
 
Mimi naomba kujuzwa jinsi nitaona vitu vyangu nilivyohifadh katika flash,mana ghafla sivioni,na capacity ni 32Gb,free space unasoma 16Gb,
Msaada tafadhal nafanyaje kuweza kuona vitu vyangu?

thA God thA bubbs!!
 
Mimi naomba kujuzwa jinsi nitaona vitu vyangu nilivyohifadh katika flash,mana ghafla sivioni,na capacity ni 32Gb,free space unasoma 16Gb,
Msaada tafadhal nafanyaje kuweza kuona vitu vyangu?

thA God thA bubbs!!
Fungua flash yako nenda tab ya juu pale click 'view' then nenda hidden weka tick! Basi utayaona mafaili yako! Usipoyaona ujue hayapo

Million dollars
 
Kila mtu ana njia ambayo anaona ni rahisi.. mie kwa upande wangu kutengeneza bootable flash disk kwa kutumia power iso ni simple pia ni the best.
Power iso ndo mpango mzima ni very simple

Million dollars
 
Kila mtu ana njia ambayo anaona ni rahisi.. mie kwa upande wangu kutengeneza bootable flash disk kwa kutumia power iso ni simple pia ni the best.
Power iso ndo mpango mzima ni very simple

Million dollars
 
Back
Top Bottom