Jinsi ya kutafuta corrupted file

Jinsi ya kutafuta corrupted file

Joined
Oct 17, 2016
Posts
46
Reaction score
47
Hakuna kitu kinachokera kwenye matumizi ya computer kama kupokea ujumbe au sauti kuwa kuna file ime-corrupt kwenye computer yako.
najua wengi sana hatuelewi ni njia gani ya kuweza kutafuta hyo file na mwisho huishia kubadilisha WINDOWS. sometimes kubadilisha windows inakuwa sio solution coz unaweza kubadilisha window na bado ukakutana na tatizo lile lile. hapa nimekuwekea njia mbili zitakazo weza kukusaidia kutafuta hyo corrupted file na kuweza kufix tatizo lake

---> KUTUMIA COMMAND
♧ funga program zote na kisha RESTART computer.

♧ wakati tu computer imeanza KU - RESTART bonyeza F8 kwenye keyboard. kama utakavyoona kwenye maelezo kwenye screen. lengo ni kuiingia kwenye SAFE MODE kama utaona option ya SAFE MODE wakati wa kufunguka basi ingia hapo

♧ baada ya kukamilika kufuka kwa SAFE MODE nenda kwenye My Computer kisha right click kwenye Drive ambayo ndio kuna corrupted file (kutokana na ujumbe uliopokea) kisha bonyeza PROPERTIES ya hyo drive

♧ bonyeza kwenye TOOLS kisha utabonyeza kwenye CHECK NOW (inayopatikana hapo kwenye “Error-checking”).

KUMBUKA: itachukua muda kutafuta kulingana na ukubwa wa hard disk yako

♧ baada ya kumaliza kuscan nenda kwenye START BAR kisha fungua RUN

♧ kwenye RUN dialog utaandika ( sfc/scannow) bila bracket kisha bonyeza OK

hii ni sawa na njia ya scan now isipo kuwa hii inaangalia kiundani zaid mpka zile file ambzo zisingeweza kuonekana na CHECK NOW

♧ baaka ya kumaliza hapo ni kufanya system restore

♧ ingia CONTROL PANEL kisha tafuta sehem ya “Recovery”

♧ bonyeza kwenye “Open System Restore” kisha fuata maelezo

hapo itakuwa umemaliza tatizo lilokuwa lina sumbua computer yako

---> KUTUMIA SOFTWARE
kuna software nyingi zipo ambazo zinaweza kusolve tatizo lako kama hz

- File Cure
- RegCure Registry Cleaner
- PC Tools Spyware Doctor with AntiVirus 2011

unaweza kuchagua moja kati ya hzo hapo juu fuata maelezo ya kila moja ili kujiridhisha kwenye ufanyi kazi wake

NB: ikiwa kuna tatizo lolote kwenye computer yako..usisite kutupigia kwa namba 0676040772..na kwa mahitaji ya kununua vioo vy computer,hard disk,ram,processor mnakaribishwa
 
Back
Top Bottom