KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 10,569
- 21,075
Sitawafunza kila kitu lakni hizi tambi zinapendwa na kila MTU wew mama wa nyumbani ukipika tambi za dengu ukapakia kwenye vifungashio utapata faida kwa hiyo pesa ya mahitaj madogo madogo inaweza kukusaidia ukizingatia wew Fanya biashara zinazo baki kula na familia yako maana ni tamu sana😛..
Ukiwa na mashine yake kupika ni rahisi sana raha zaidi changanya na karanga
JINSI YA KUPIKA TAMBI ZA DENGU
MAHITAJI
1. Unga wa dengu ½ kilo
2. Binzari nyembamba ½ kijiko cha mezani
3. Unga wa pilipili manga kijiko 1 cha chai
4. Unga wa mchele ¼ kilo
5. Chumvi kiasi
6. Mafuta ya kula ½ lita
7. Baking powder
JINSI YA KUPIKA
1. Changanya unga wa mchele pamoja na ule wa dengu. Kisha chukua nyunyuzia baking powder na baadaye chumvi. Weka unga wa binzari nyembamba na pilipili manga.
2. Baada ya hapo changaya vizuri na kisha weka maji kidogo kidogo huku ukiukanda hadi liwe donge gumu kama unavyofanya kwenye maandazi. Baada ya hapo weka donge lako pembeni na funika. Acha likae kwa muda wa nusu saa hadi saa moja.
3. Baada ya hapo chukua karai la mafuta weka jikoni acha hadi mafuta yapate moto kabisa.
4. Kisha chukua mashine ya kupikia tambi na weka donge lako. Kandamiza taratibu huku ukiruhusu minyororo ya tambi kuingia kwenye mafuta yaliyo jikoni.
5. Weka kiasi kiasi huku ukikaanga. Acha mpaka zitakapokuwa zimeiva na kukauka vizuri. Epua na weka pembeni. Weka kwenye sahani safi na kavu. Tambi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.