Mwanampuna
Senior Member
- Jul 21, 2016
- 131
- 80
Mahitaji
1.Viazi mbatata kilo 1
2. Mabamia fungu 1 kubwa
3. Mabiringanya makubwa 2
4. Karoti
5. Mafuta ya kupikia
6. Nyanya
7.Vituungu maji 2
8. Swaumu
9. Ndimu
10. Chumvi
Jinsi ya kupika
1. Chukua viazi vimenye na uvioshe kisha vipasue mara nne kwa urefu kisha uvikate kwa upana kama unakata cripsy weka kwenye chombo chake
2. Kisha chukua biringanya litoe lile ganda lake la juu la kijani lakini usilimenye maganda kisha lipasue kama ulivyofanya kwenye viazi weka kwenye chombo chake
3. Chukua bamia likate vipande vidogo kisha weka kwenye chombo chake
Kisha bandika kikaangio weka Mafuta hadi yapate moto kisha weka vile viazi vikaange kama unavyokaanga chipsi na hakikisha visiwe vitepe kisha weka kwenye bakuli
4. Kisha kaanga mabiringanya hadi yawe brown kidogo (yakizidi brown yanakua machungu) kisha uweke kwa juu ya vile viazi ulivyovikaanga
5. Chukua bamia kaanga hadi ziwe brown kisha weka juu ya zile biringanya na viazi ulivyovikaanga
6. Pika mchuzi mzito kama rosti hakikisha unautia vitunguu swaumu, karoti na ndimu na viungo vyote vya mchuzi. Kisha mwagia mchuzi wako kwenye ule mchanganyiko wako wa viazi ,biringanya na bamia ulizokaanga
Unaweza kula mboga hii kwa chapati au maandazi