Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 278,618
- 1,128,609
MAHITAJI
1.Karanga za kusagwa
2.Chumvi
3.Unga wa mlenda
4.Maji
Jinsi ya kuandaa
Chukua karanga zilizosagwa vizuri loweka kwenye bakuli la maji,baada ya muda anza kuzikoroga utokee uji mzito kiasi
Bandika sufuria lako jikoni hakikisha moto sio mkali,maana moto mkali unawahi unguza mboga
Baada ya hapo mimina ule uji wa karanga kisha koroga taratibu mpaka uchemkie(ukiacha kukoroga utaungulia kwa chini)
Uji ukishachemkia(kutokota au kupogoma)weka unga wa mlenda unaweza weka vijiko vya chakula vitatu(hapa ni kulingana na mahitaji yako usiukoleze sana mlenda kwa kujazia unga wake.
Kisha weka chumvi
Koroga kama unasonga ugali,usitumie nguvu sana ni rahisi tu
Baada ya hapo epua,mlenda wako tayari.
NB: sina utaalamu sana wa vipimo vya upishi,ndio maana sijaweka vipimo sahihi vya upishi huu