zigi 01
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 323
- 198
Mimi ni kijana, ninataka nifungue biashara ya urembo sehemu fulani. Nimeshapata fremu ya duka but bado sijajua utaratibu wa kupata Leseni ya Biashara ili niweze kuanza kuuza bidhaa zangu
Michango
Michango
Mkuu ungempa taratibu kuanzia mwanzo hadi kupata hiyo leseni. (Samahani sio nakukosoa bali naboresha maelezo).
Kwanza aende TRA apate TIN namba ambapo kule ili apate TIN namba inamlazimu kuchukua zile fomu za makadirio ya kodi, barua ya kupeleka kwa mwenyekiti wa serikali za mitaa, mkataba wa hilo eneo lake la biashara na asisahau passpoti size vlvl igongwe muhuri juu yake na Mwenyekiti. Hii ni TIN namba ya biashara
Baada ya kupata hiyo TIN namba toka TRA inabidi aende manispaa ya sehemu husika atapewa fomu ambapo atajaza na kuambatanisha kopi za mkataba wa eneo la biashara, TIN namba na chochote muhimu kutokana na biashara anayofanya kama itakuwa biashara maalum. Lakini biashara ya kawaida mara nyingine huwa wanataka na cheti cha afisa afya au sehem ajaze nk.
Kwa biashara maalum kama biashara ya madawa watataka na cheti cha TFDA nk