Jinsi ya kupata GPA kubwa uwapo chuoni

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,545
Habari zenu wanaJF,

Binafsi namshukuru sana mwenyezi Mungu kwa uhai na afya anayozidi nineemishia. Na nipende kuwapa pole wale wote wanaopitia maswaibu mbalimbali na kumuomba Mungu awapiganie katika majanga hayo yanayowapata.

Bila kupoteza wakati, niende moja kwa moja kwenye lengo la uzi huu kama linavyojieleza hapo juu.

Kuna mambo ambayo ili ufanikiwe ni muhimu kufuata ushauri kwa watu ambao wamekutangulia kwa namna moja au nyingine.

Ushauri huu utawafaa zaidi wanafunzi wanaotegemea kuanza masomo yao mwaka huu wa elimu.

Zifuatazo ni mbinu ambazo zitakusaidia kufaulu vizuri masomo yako na kupata GPA kubwa itakayokuwezesha kufit katika soko la ajira na kukupatia fursa mbalimbali kama scholarships:

1. Hakikisha haukosi kipindi hata kimoja ( lectures pamoja na semina au practicals).

Jitahidi usikose kipindi chochote kwani kipindi kimoja cha dakika 40 au 80, mwalimu anaweza kufundisha sehemu kubwa sana.

Na kuna baadhi ya sehemu kuelewa vizuri lazima usikie sauti ya mwalimu. Ukiachana na hilo, walimu wengi wanaweza toa quizzes kwenye vipindi vyao bila taarifa yoyote.

Hivyo kama haukuwepo utakosa marks za bure.Kumbuka kwa ngazi ya chuo kikuu kila marks hata 1 inamchango mkubwa sana wa kukutengenezea GPA nzuri siku ya mwisho.

Semina ni za muhimu sana. Usipuuzie maana luna sheria zinazosema usipouzulia semina kwa mfululizo unaweza fukuzwa chuo.

2. Tumia Muda mwingi kusoma.

Kitu kikubwa kilichokupeleka chuo ni kutafuta elimu. Hivyo basi, hakikisha kwa Siku unatumia angalau masaa manne ya kujisomea. (Usihesabie masaa ya vipindi)

Kwa uzoefu wangu, nilikuwa nasoma lisaa limoja then napumzika dakika kumi, then napiga tena lisaa limoja. Nikishakamilisha masaa mawili ninapumzika kabisaa mpaka masaa mengi yapite.

Fanya urafiki na maktaba. Uzulia sana maktaba kuliko cafeteria. Jitahidi kupitia reference books za kozi unayosoma.

Asilimia kubwa ya mwalimu hupenda kupima sana wanafunzi kama wanafuatiliz reference wanazozitoa. Ukiingia internet jaribu kugoogle mambo yanayoendana na kozi unayosoma darasani.

Ukiwa free kaa chini anza kuwaza uliyosoma darasani Hii itakusaidia sana.

3. Heshimu walimu wako na wanafunzi wenzako.

Tofauti na hatua zingine za elimu, kwa level ya chuo hasa hasa chuo kikuu, mwalimu ndio kila kitu kwenye maamuzi ya mithiani na matokeo.

Usitengeneze bifu na walimu wako. Ukikutana na mwalimu asie na hofu ya Mungu na ukaingia kwenye anga zake, atakufanya kitu mbaya sana.Shirikiana na wanafunzi wenzako.

Chagua marafiki wa kusoma nao pale unapoona kuna uhitaji wa majadiliano. Chagua watu walio sahihi na shiriki katika shughuli zote kilamilifu.

4. Usiingie kwenye mahusiano kama bado hujakua kihisia.

Takwimu zinaonesha wengi wabapojiunga na chuo kikuu uanza kwa ufaulu mkubwa sana Ila wanapozoea mazingira ya chuo ya uhuru kupitiliza wanajisahau na kuanzisha mahusiano ambayo kwa njia moja au nyingine huwapelekea kushuka kitaaluma.

Mimi binafsi, niliingia kwenye mahusiano kichwa kichwa, yaliyonikuta kwa kweli yalinirudisha nyuma sana kitaaluma. Rafiki yangu mmoja alifukuzwa chuo(discontinued) na baadae alijiua kisa mahusiano.

Hivyo, kuweni makini sana na mahusiano ya kimapenzi. Kama huwezi himili mikiki ya kuachwa nakushauri achana na wadada wa chuo.

Usiwekeze muda wako na mali katika mabinti wa chuo kama hauna uhakika na upana wa moyo wako.

Ikitokea mahusiano yamekuchanganya sana mpaka kufikia hatua ya kukurudisha nyuma kitaaluma omba ruhusa ya kuhairisha mwaka wa masomo ili mwakani uje uendelee kuliko kufa kisabuni huku ukiporomosha tofali za GPA.

5. Mtegemee Mungu sana.

Yote yaliyotangulia ni ya ziada. Kikubwa nikumtegemea Mungu kwani yeye ndio chanzo cha akili. Binafsi nilimtegemea Mungu kwa sababu bila Mungu, afya inaweza zorota na kupelekea kuyumba kitaaluma.

Uhai pia tulionao sio matokeo ya kutunza afya zetu Bali ni matokeo ya Neema na Rehema za huyu Mungu.

Jiunge na vikundi vya dini vilivyopo chuoni kwako kama vile USCF, TUCASA n.k. Vikundi hivyo ni sawa na alarm itakayokuwa inakuamsha pale utakapokuwa imelemewa na anasa na Uhuru wa chuo na ukumbusha kuwa chuoni ni kupita tu bado safari ndefu mbele.

Kwa upande wangu Mimi, Mungu amenisaidia sana, uhai na afya nilipokuwa chuo, japokuwa kuna kipindi niliugua yeye alinisaidia katika masomo yangu.

Hata kama nilikosa vipindi kwa sababu ya afya. Mungu alizipa nafasi.

NB. Tumia muda wako vizuri, ya Mungu mpe Mungu na ya Kaiser mpe Kaiser. Kuna watu wataacha vipindi vyao eti kiss anaenda sijui kuimba au kufanya vitu ambavyo sio muda wake. Ndugu zangu, jitahidi usiwe mtumishi katika level ya kusahau majukumu yako mengine. Uta discontinue!!!

Mtolee Mungu wako zaka au sadaka kama unaamini atazipokea kupitia watumishi wake. Hii pia ni siri nyingine ambayo mimi binafsi inanisaidia sana.

ASANTENI
Mungu awabariki muwapo masomoni.
 
Well Said mkuu,
Iakini hakunaga mtu anaeombea mabaya yamkute katika kipindi cha masomo, bali huwa hivi vitu

vinakuja by default unajikuta umefeli, ama umeshindwa timiza malengo yako

Na sababu zinakua ni nje na ulizotaja
Nakubaliana na wewe mkuu,
Lakini nikuhakikishie kuwa asilimia 90 ya kufeli au kufaulu masomo ya chuo huwa ni uzembe na kupuuzia mambo. Ni wachache sana huwa inatokea by default.
Mimi naamini MTU mpaka kufikia level ya chuo ana akili.
 
Nebuchadinezzer,

Pamoja na yote hayo kama huna IQ kubwa pia genetically, first class itakuwa mtihani!

Unaweza pata,ila genetics zina play part kubwa sana!

Nilikuwa na wanangu wana juhudi sana wanalala darasani na wanafanya kila kitu!

Homeworks zote, tests zote kila kitu, bado genetically brain cells zao sio sharp inavyotakiwa!
 
Kupata GPA kubwa inategemea MTU na MTU na akili yake maana kuna watu nilikuwa nasoma nao yaani kutwa discussion hawakosi, vipindi ndo usiseme hawamic lakini nikuambie matokeo yao yalikuwa yakawaida sana....enzi zangu kwanza nasoma nikishasikia paper limetangazwa yaani hapo unaanza kujiandaa week mbili kabla ya paper na hapo unapitia past paper na notes za lecture ukiwa mzuri wa kukariri we kariri utaelewa ukishagraduate na ndo nilichokuwa nakifanya mwishowe tumetoka na GPA yetu safi kabisa ya 4.0 wale wazee wakukesha wapo kwenye 2.8-3.4 Ila sio wote wanaokesha wanafanya vibaya Ila asilimia kubwa wanafanya vibaya....
PIA USIENDEKEZE DINI SANA KATIKA MAZINGIRA YA KUSOMA, TENGA NUSU SAA AU SAA NZIMA YA KUSALI NA SIO MASAA MENGI UNATUMIA KUSHINDA MAKANISANI AU KWENYE MIKUTANO MJOMBA GPA KUBWA UTAISIKIA MASIKIONI
 
Unaweza cha msingi angalia ratiba ya vipindi na ratiba yako ya kujisomea Ila kwa biashara unayoweza kufanya sio ile ya kukaa ni yakutembeza mfano kuwauzia vitu wanachuo wenzako nyakati za usiku lakini ukisema ufungue duka umuweke MTU au ukae mwenyewe utapata shida sana Guy Isaac
 
Mi nafikiri %kubwa ya kufeli ni ukilaza tu. Labda kupata GPA kubwa ndio changamoto unabidi uzikabili kama wewe ni kichwa cha kawaida.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom