Smart Technician
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 653
- 829
Naomba summary
Binadamu tunategemeana katika mambo mengi ikiwemo kupata furaha.Naomba summary
Shukrani kiongoziBinadamu tunategemeana katika mambo mengi ikiwemo kupata furaha.
Furaha ya maisha yetu mara nyingi inategemea jins tunavyointeract na wenzetu so tusipende kujitenga inaleta upweke
Sent using Jamii Forums mobile app
Furaha ni tunda (zao) la Roho MtakatifuBiblia. Wagalatia 5:22-23
[22]Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
But the fruit of the Spirit is love, joy, peace, longsuffering, gentleness, goodness, faith,
[23]upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Meekness, temperance: against such there is no law.
Hii nilikua sijajua siku nilipo ijua nimekua na furaha sana kutangamana na watu.Siku moja kundi la watu 500 walikua wamehudhuria Semina. Mara msemaji mkuu wa semina hiyo akaanza kumpa kila mtu puto (balloon), na kuwaambia kila mmoja aandike jina lake juu la puto alilopewa. Kisha maputo yote
yakakusanywa na kuwekwa kwenye chumba kimoja.Kisha watu wote wakaambiwa waingie kwenye chumba hicho na kila mmoja atafute puto lenye jina lake ndani ya dakika 5. Kila mmoja akaanza kuhangaika huku na kule akitafuta puto lake bila mafanikio, na chumba chote kikawa na fujo tupu.
Baada ya dakika 5 kwisha, hakuna hata mmoja aliyekua amefanikiwa kupata puto lake. Ndipo msemaji akawaambia basi kila mmoja achukue puto lolote tu na ampe mtu ambaye jina lake limeandikwa kwenye puto hilo. Ndani ya dakika chache kila mmoja akawa ameshapata puto lake.Ndipo msemaji mkuu akasema:
"Hii inatokea kwenye maisha yetu kila siku. Kila mtu anahangaika kutafuta furaha yake huku na kule, bila kujua ilipo. Furaha yako ipo kwenye Furaha za watu wengine. Wape furaha watu wanaokuzunguka;nawe utapata Furaha yako.Usipende kujitenga... Maisha ni watu.... Bila watu hakuna furaha....hakuna Maisha! Sambaza upendo.. [emoji253][emoji253][emoji259][emoji259][emoji259]