Jinsi ya Kuondoa Lock Pattern ama Password Uliyoisahau katika Android

The Certified

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
910
774
Makala hii itakusaidia kuweza kuondoa pattern ama password (nywila) uliyosahau katika simu yako (Android), zipo njia nyingi kutegemea na aina ya simu au toleo la Android ambalo simu yako inatumia.
Kwa kutumia barua pepe yako na password ya akaunti ya Google.
Simu zote ambazo zinatumia Android Kitkat ambayo ni toleo la 4.4 na nyingine zote ambazo ni matoleo ya nyuma ya hili zenyewe ni rahisi pindi unaposahau password yako, katika kundi hili la simu pindi tu unaposahau pattern ama password yako simu yako itakutaka uingize barua pepe na password yako ya Google ambayo ulijiandikishia katika simu hiyo na kisha simu yako itafunguliwa.
Angalizo! njia hiyo itafanya kazi iwapo umewasha data katika simu.
Kwa kutumia Android Device Manager.
Njia hii simu zote ambazo katika zimewezeshwa programu hii, vile vile njia hii itafanikiwa iwapo tu wakati huo intaneti ya simu itakuwa imewashwa. njia hii inaweza sio tu kubadilisha password ya simu kwenda katika password yako mpya ila pia inaweza kusaidia kufuta mafaili yote yaliyo ndani ya simu โ€“ hii ni muhimu kama simu imepotea au kuibiwa.
Fuata hatua zifuatazo kufungua simu uliyoifunga.
1. Tembelea google.com/android/devicemanager kupitia katika simu nyingine ama kompyuta
2. Ingia kwa kutumia barua pepe pamoja na password yako uliyotumia kusajilia katika simu iliyojifunga
3. Tafuta na chagua kifaa ambacho unataka kukifungua (maana kama una vifaa zaidi ya kimoja ulivyo visajili katika huduma hii vyote vitaonekana hapa)
4. Chagua Lock na uinigize password ya muda kisha bonyeza Lock tena
5. Baada ya hapo unatakiwa uone meseji ikithibitisha kuwa kufaa chako kimebadilishwa password
6. Wakati huu katika simu utaona sehemu ya kuandika password inatokea hapa jaza ile password yako mpya.
7. Ingiza pasword na uende moja kwa moja kuiondoa pasword hiyo ya simu yako.
Kufungua simu kwa Apps mbali mbali.
Watengenezaji mbali mbali wa simu wanakuwa na application zao binafsi kwaajiri ya kusaidia kufungua simu iliyojifunga na password kusahaulika, siku zijazo tutaiongelea kwa marefu njia hii kwa undani. Kwa ufupi ni kwamba njia hii inafanya kazi kama njia iliyopita tofauti ni chache na zinatokana na ukweli kwamba zinatengenezwa na watu tofauti.
Kufungua simu kwa kurudisha industrial default settings
Njia hii hufuta kila kitu katika simu na kuifanya iwe na mpangilio ule ule iliokuwanao wakati inatoka kiwandani. Njia hii ni ndiyo kimbilio la mwisho kwa ikiwa kama mtu umesahau pattern na password, njia hii hufuta mipangilio yoote ya simu na hifanya simu iwe kama mpya na kufuta passwords ama patterns zilizo katika simu.
Makala zinazofuata nitaandika kipengele kimoja kimoja kwa kirefu zaidi. Tuambie je wewe ulitumia njia ipi kuondoa pattern ama password kwenye simu yako
 
Ninaswali dogo.

Iwapo simu imeibiwa na ndani ya dakika chache wakaislashi kanbla hujapata device nyingine na kulogin kwenye google account

Je utakuwa bado na uwezo wa kubadili password na ku futa data zako?
 
Ninaswali dogo.

Iwapo simu imeibiwa na ndani ya dakika chache wakaislashi kanbla hujapata device nyingine na kulogin kwenye google account

Je utakuwa bado na uwezo wa kubadili password na ku futa data zako?
Ndio Mkuu uwezekano upo
 
kama un a software/box ya mirracle box kuna option inasema ''open developer option'' then rud kwenye aina ya kifaa click read pertern code, au password kisha click start subiria itakuonesha katika pc au simu ikiunlockiwa partern kwenye pc itACHORA NA KUWEKA POIT 1 TO END
 
Dah ndugu sasa hivi kwa simu za android latest hata ukifanya hard reset au wipe device bado itakwambia tu kuwa simu yako imefanyiwa reset na kukutaka utumie email iliyowekwa wakati ukiifanyia settings mara ya kwanza. Kama huna hizo details, utachemsha mbaya ndugu
 
Bado Kuna watu wanatumia tu kitkat ? njia zenu zko outdated hazi break SE LINUX implementation kwenye latest os
 
Dah ndugu sasa hivi kwa simu za android latest hata ukifanya hard reset au wipe device bado itakwambia tu kuwa simu yako imefanyiwa reset na kukutaka utumie email iliyowekwa wakati ukiifanyia settings mara ya kwanza. Kama huna hizo details, utachemsha mbaya ndugu
Inaitwa FRP tunaweza iondoa fast. njoo inbox
 
huyu atakuwa hatari lock uweke ww harafu usahau ni shida au ni password ya email mkuu au
 
Kila nikibonyeza power button na volume+ kuna kidude cha android kinakuja na kinaandika 'no command. Mnisaidie wadau ili ni wipe data.
 
Back
Top Bottom