Jinsi ya kumudu mapenzi ya mbali...

Jinsi ya kumudu mapenzi ya mbali...

ricktz

Member
Joined
Jun 25, 2016
Posts
20
Reaction score
11
Na FREDRICK KISALALA

Siku zote mapenzi huyapa maisha thamani lakini wapo ambao hujikuta kwa namna moja ama nyingine wanatengana na wapenzi wao kwa sababu tu ya mihangaiko ya kila siku ya kujitafutia riziki. Masomo na wakati mwingine utengano huwa ni matokeo ya wapendanao kuishi sehemu tofauti. Hii huwakumba sana wanafunzi wa vyuo na shule za bweni (hostel).

Umbali hulifanya penzi baina ya wapendanao kuteteleka kama wapendanao hawatafanya kazi za ziada kuhakikisha wanaziba mianya yote itakayosababisha usaliti kama sio kuachana kabisa, Hata hivyo, mapenzi ya mbali huna ni vigumu kuteteleka endapo tu wapendanao wanamapenzi ya dhati na kutamani kuwa pamoja kila wakati na mmoja wapo kuamua kujitoa muhanga kwa kuamia anakoishi ama anakofanyia kazi laazizi na mwandani wake.

Pamoja na hayo yote bado umbali hauwezi kuwa ni tatizo kubwa sana la kutetelesha uhusiano wako na mpenzi wako. Mnaweza kudumisha mapenzi yenu ya mbali endapo utafanya haya.

MAWASILIANO MARA KWA MARA

Mawasiliano ni nguzo muhimu sana baina ya wapendanao, humfanya kila mtu kuhisi uwepo wa mwenzi wake hata kama atakuwa mbali naye. Hivyo, kama una mpenzi wako aliye mbali nawe hakikisha unakuwa naye karibu kwa kumtumia ama sms, email, kadi au simu.

Aidha, pindi mnapowasiliana hakikisha humkwazi mwenzako kwa namna yoyote ile, kwani kuna watu wengi wanatabia ya kudharau baadhi ya mambo kutokana na kutingwa na shughuli kadha wa kadha, naomba nikuweke wazi kuwa hata kama umebanwa vipi pindi mpenzi wako aliye mbali anapokutumia ujumbe kwenye simu yako basi usisite kumjibu katika muda muafaka na siyo kuuchuna hadi ulalamikiwe.

HESHIMU HISIA ZAKO

Mapenzi ya kweli yametawaliwa na hisia kali ambazo ndizo huwafanya wapendanao kufikishana kwenye mambo fulani kwani pasipo hisia hata uwe na ujuzi au utundu wakutosha hutapata raha ya mapenzi, Kama kweli unampenda kwa dhati mwenza wako na mmetengana kutokana na sababu za kimasomo ama kazi kwa hakika utakuwa tayari kumtunzia penzi lake hadi mtakapokutana tena.

Uaminifu pekee ndio utakaokufanya uwasiliane mara kwa mara na mwenza wako na kwenye uaminifu mapenzi hushamiri huku kila mmoja akimuonea wivu wa hapa na pale mwenzi wake (lakini sio ule wakubomoa!) Hivyo heshimu hisia zako kama kweli unampenda mwenzi wako kwa kumuonesha unampenda.
9aa4d37cd8c8ccd1a482ff2ed91a5f6c.jpg

UMBALI ISIWE KIGEZO KUNYIMANA

Mpe mwandani wako raha kamili kama ilivyokuwa awali mlipokuwa pamoja! Bila shaka unajiuliza inawezekanaje? Hili linawezekana kwa kutumia njia yoyote ya mawasiliano. Mfano kama nyote mna simu jiandae vya kutosha nikiwa na maana uhakikishe upo sehemu ambayo utakuwa huru kuongea ama kufanya chochote Kitakachokufanya uhisi raha isiyo na kifani na kukufikisha kwenye kilele cha mlima kilimanjaro bila kutarajia.

Bila shaka kila mtu anamfahamu vema mpenzi wake na hasa nini hupenda kufanyiwa ili awezekufika safari yake na kama ndivyo basi hakikisha unafanya mambo yote ambayo ukimfanyia mwenzi wako pindi mnapokuwa kwenye mambo fulani hupagawa.
 
Naomba uzoefu binafsi hapa, kwa wale wenye wapenzi (ambao bado kuoana) na wale ambao tayari wapo kwenye ndoa.

Ni jinsi gani mnaweza kufurahia mapenzi yenu ili hali hampo karibu? Najua inaweza kuwa rahisi kwa baadhi yetu, lakini kwa wengine ikawa ngumu sana kustahamili ile hali ya umbali, wivu pia unaweza kutawala mapenzi, ugomvi usioisha n.k.

Pia inawezekana watu wakatumia mitandao na video calls kuonana mubashara na wengine wanasaidiana kwa namna wanazojua wao kupunguza ashki kwenye hizo video calls.

Je, nani anaumia zaidi kihisia, yule anayeachwa nyumbani "Tanzania" au yule aliyepo ughaibuni??

592816f58dccb0e56e75bacf5972b578.jpg
 
Anaeachwa(Tanzania) Mara nyingi ndo anaumia zaidi kihisia.

Na sio lazima kuachwa nyumbani Tanzania..mnaweza kua wote mpo ughaibuni mmoja akatangulia nyumbani.kwa hapa Sina uhakika Sana Ila Kama mlipendana kiukweli Yule anaetangulia ataumia kukuacha ughaibuni mwenyewe,Ila Kama ilikua Ni pass time tuu hakuna upendo wa ukweli,anaetangulia ataona poa tuu Tena atafurahia huo utengano(easy break up)
 
Mara nyingi aliye UGHAIBUNI ndy anaumia zaidi....sababu MFANO mwanamke... Au mwanaume akiwa. Hapa nyumbani.. Utapata habari zake nyingi sana kupitia FRIENDS.. au jamaa...YAANI utasikia uzushi mwingi sana..especially kwa sisi MABAHARIA. ..tunakutana nayo hayo...usipokuwa makini unaweza ukaacha kila kukicha..mara nyng MUHUSIKA akiwa hayupo karibu na MPENZI wake..wanajitokeza SPY wasio na malipo..kumchunguza nyendo zake MKE..au MUME...pia kuna wale waliokuwa wanahofia kumfatilia MKEO wakati mumuwe yupo.. Nao ndy wakati wao KUSUMBUWA....yupo jamaa yangu mmoja alikufa kwa KIHORO TU...ilikuwa kila akipiga simu... Akishamaliza kuongea ananifunika BLANKET analia tu
Kwa jinsi anayoyasiki ya mkewe.... Mara hapokei sm..mara simu hapokei...mara inaktwa
.akipiga kwa friends anakutana na STORY MPYA mara mkewe yupo nar na friend fulani..mara kaonekana na jamaa anarudishwa asubuhi.. Mradi tu New story..kila kukicha.... Jamaa alipunguwa uzito mwishowe akafa GHAFLA TU....mm nasema ni bora yeye awe UGHAIBUNI.. MWANAUME awe nyumbani.. Mara mia..hutojuwa nini kinafanyika huko....
 
Umeandika nini sasa, maana unamaanisha anayeumia ni mwanamme tu
 
Umeandika nini sasa, maana unamaanisha anayeumia ni mwanamme tu
. Nina maana anayebaki nyumbani ndy anamuumiza zaidi aliye UGHAIBUNI... Maana aliyeko UGHAIBUNI ni ngumu kujuwa anachofanya..lakini atakayebaki nyumbani ni rahisi kujuwa nyendo zake zote..kuanzia siku umeondoka... Ni rahisi watu kumfatilia mtu ambaye mpnz wake hayupo kuliko mpnz wake akiwepo hapo..mm nimekupa mifano ya watu ambao husafiri mara kwa mara na kuwa mbali na wapenzi wao...ila Atakayebaki nyumbani ndy ananafasi kubwa ya kumuumiza mwenzie....mifano mingi tunaioana Jamaa anarudi.. Either anafumania
..au anakuta mke au mume kaoa au kuolewa n mtu mwingine...lakini ngumu sana kuona mke au mume karudi na mpnz mwingine UGHAIBUNI..
 
Anaeachwa(Tanzania) Mara nyingi ndo anaumia zaidi kihisia.

Na sio lazima kuachwa nyumbani Tanzania..mnaweza kua wote mpo ughaibuni mmoja akatangulia nyumbani.kwa hapa Sina uhakika Sana Ila Kama mlipendana kiukweli Yule anaetangulia ataumia kukuacha ughaibuni mwenyewe,Ila Kama ilikua Ni pass time tuu hakuna upendo wa ukweli,anaetangulia ataona poa tuu Tena atafurahia huo utengano(easy break up)
Hata mimi naona havyo, anayeachwa home anakuwa na mawazo sana.

Halafu, mbona naona mahusiano mengi ya wanaoenda na kuwaacha wenzao home yanaishia kuumizana tu?
 
Mara nyingi aliye UGHAIBUNI ndy anaumia zaidi....sababu MFANO mwanamke... Au mwanaume akiwa. Hapa nyumbani.. Utapata habari zake nyingi sana kupitia FRIENDS.. au jamaa...YAANI utasikia uzushi mwingi sana..especially kwa sisi MABAHARIA. ..tunakutana nayo hayo...usipokuwa makini unaweza ukaacha kila kukicha..mara nyng MUHUSIKA akiwa hayupo karibu na MPENZI wake..wanajitokeza SPY wasio na malipo..kumchunguza nyendo zake MKE..au MUME...pia kuna wale waliokuwa wanahofia kumfatilia MKEO wakati mumuwe yupo.. Nao ndy wakati wao KUSUMBUWA....yupo jamaa yangu mmoja alikufa kwa KIHORO TU...ilikuwa kila akipiga simu... Akishamaliza kuongea ananifunika BLANKET analia tu
Kwa jinsi anayoyasiki ya mkewe.... Mara hapokei sm..mara simu hapokei...mara inaktwa
.akipiga kwa friends anakutana na STORY MPYA mara mkewe yupo nar na friend fulani..mara kaonekana na jamaa anarudishwa asubuhi.. Mradi tu New story..kila kukicha.... Jamaa alipunguwa uzito mwishowe akafa GHAFLA TU....mm nasema ni bora yeye awe UGHAIBUNI.. MWANAUME awe nyumbani.. Mara mia..hutojuwa nini kinafanyika huko....
Ni ngumu sana kuacha familia, mke na watoto kwenda ughaibuni.

Ningependa kupata experience ya wale walioacha wake/waume zao na kutimkia ughaibuni kimasomo/kikazi.

Wana-manage vipi?
 
Ukiwa mbali na umpendaye lazima uumie haijalishi upo wapi
Kuna tofauti ya wewe upo Dar mwenzako yupo Mwanza na yule yupo Manhattan na wewe upo Arusha, wewe huioni tofauti??
 
Ni ngumu sana kuacha familia, mke na watoto kwenda ughaibuni.

Ningependa kupata experience ya wale walioacha wake/waume zao na kutimkia ughaibuni kimasomo/kikazi.

Wana-manage vipi?
Mkuu ni hatari mno KUACHA family na kwenda ughaibuni..wengi wanaishia kwa VILIO tu..na ndoa kuvunjika... MIMI nina jamaa yangu akuta mkewe ana mtoto mchanga...wakati kakaa ughaibuni miaka 3""aliporudi...jasho lilimtoka
 
Hata mimi naona havyo, anayeachwa home anakuwa na mawazo sana.

Halafu, mbona naona mahusiano mengi ya wanaoenda na kuwaacha wenzao home yanaishia kuumizana tu?
Unapoenda huko ughaibuni Mara nyingi unakutana na wa Aina yako ambae unajikuta una furaha nae zaidi ya ulokua nae mwanzoni. Mawasiliano yatapungua na wa nyumbani,nae atahangaika na wapembeni.
Ukirudi nyumbani mtihani,unachanganyikiwa ufanyeje.
Ni kuombea tuu kuelewana lasivyo wa ughaibuni,uliemuacha home, wote unawapoteza...
Mi nnaona ukienda nje confusions Ni nyingi kimahusiano kipindi unarudi home..watu wawe tuu honest popote wanapokua.itapunguza sintofahamu nyingi ukirejea nyumbani .
 
Back
Top Bottom