Jinsi ya kumtuliza mume wako siku ya weekend

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,743
25,535
Siku hizi wa naume licha ya kukimbia nyumba zao
kwa kisingizio cha kazi maajabu week end hasa
Jumamosi utasikia wanaaga nafika hapo njiani
naja naenda kununua gazeti.

Kumbe wanaenda kunywa supu unasubiri wee
mpaka alasiri au jioni. Hivyo wanandoa wengi hili limekuwa tatizo
mwanaume kiguu na njia asubui mchana na njia
kumuacha mama na watoto.
Nini kifanyike hasa week end Mwanaume ashinde
NYUMBANI akikupumzikia??

Zipo njia nyingi mojawapo
SUPU YA WEEKEND NA MAZUNGUMZO NA MKAO
Ni kweli wanawake wengi hamjuagi kuwakalisha
waume home. Anza hivi, Siku yuko home wewe amka mapema kabla yake
fanya usafi kisha anza makeke jikoni...Mara blenda priiiii... juice... ama milk shake.....Utaona anasogea jikoni.. Wakati anakunywa juice ama milk shake...Anza kukuna nazi...Chambua mnafu...

Hapo jikoni kuna kanyama kanachemka... katia
kitunguu tupia viazi 2 na ndizi.
ile harufu ikianza kutoka utasikia anafuata maji
jikoni... kwenye friji... wala hatumi..
... utasikia nini kiko jikoni? Mmiminie supu...
Na ndizi mbili na kiazi kimoja kapilipili mbuzi
pembeni..KMA kuna chapati...Mpe.. Akimaliza supu
nakuapia atasinzia..

Akishtuka ugali na mnafu na nyama umeiva...Mpe
ale..Mshushie na glass ya mtindi...b
analewa full Hata kama kuna mama junior
anaambiwa usipige.....Baada ya hapo acha aoge apumzike... .
Kisha funga ka khanga kako kepesi jilaze
pembeni.. woiiiiiiiii..

Mkimaliza muombe pesa ya sokoni...
NAKUAPIA HATA KAMA JANA YAKE ALIKUPA
ATAKUPA TENA. jamani.... yani kwa raha ya supu... nakuapia utaambiwa
hata mama alipiga simu jana... ama utasikia
mamii.. njoo uone njoo... unaitiwa kitu cha
kwenye tv.. hahaha.

Hata hujaona mwanzo ila kwa raha yakasupu
utaitwa...Hata kama huna kalio nakuambia utapigwa kibao
hata cha mgongo.... hahahahahahahah
ahaha. Sasa wewe unaamka chai na mkate kama chuo
cha uhazili...Wali maharage kama jeshi la jwt.
Makande kama kibosho girls...Pyeeeeeeeeee.

Ataacha kuondoka akafanye yake?
Na hata akija home haupo.. uko sijui kwenye
baby shower.. mara sijui unapata wine non
alcohol na binamu yako katoka marekani she is
on the way to airport...MARA KICHAA CHA NDOA
KINAKUIMA. waiiii. Wacheni kufanya ndoa ngumu. Namaanisha.
Ni mpango kamili wa Mungu mke na mume wawe
marafiki.

Siku mume amerelax yuko tu home anazunguka
zunguka anaambiwa "Leo huna pa kwenda eee....
malaya wako kasafiri eee.." hahahaha..
Au siku mume amekaa nyumbani yani hizo hodi
uwiii...

Mashoga wanakuja huna hata muda wa
kuhudumia mume..Alafu wale mashoga uchwara.. akija anakaa
seating room na mr na kuanza oooo weka chanel 7.. saa hivi kuna series inaendelea...... nyooo....series my foot?

Yani wewe uko jikoni yeye kajiachia sebuleni tena
na miguu kapandisha kwenye sofa... hahahaha...
na kuanza kushare story na mumeo woiiiìii..
Na walivyo wachokozi wanawapigiaga wanaume
zao simu karibu na mumeo....Wanatia... oo honey
i mic you. I remember the last night... wanna kill
you next time honey...

Wewe uko jikoni unampikia mumeo wali
maharage halafu akimaliza unamuuliza leo huna pa kwenda?
jaribu siri ya supu uone.. hahahaah supu ina siri
yake. Kuna watu siku za jumamosi na jumapili nyumba
zinageuka restaurant fulani hivi... yani mpaka
raha.

Nice breakfast.
Nice lunch.
Nice dinner.. na jioni ama mchana inageuka Rest
house.... hhahahahahaha.
Baadaeeee... wanakaa kibarazani ama garden..
Kwa glass of wine non alcohol ama cold tea... ama
juice ama cofeee..```

YANI MNA MAJUMBA YA KIFAHARI LAKINI HATA
HAMUYAINJOY KWAAAAA MTAFIKIRI
MMELOGWA..
KAMA AKIONDOKA TENA NIFATE PM
 
Haya maisha bado hapo?umeyaelekeza kimaigizo zaidi.angekuepo kanumba angetengeneza clip ya ukweli.ila mumeo anakazi kwa maelezo ulivyoyashusha.
 
Hamna wanafunzi mliowapeleka shule mwezi wa kwanza huu?
Au ndoa yenu changaaaaa
 
Labda weekend moja moja sio siku zote, aache kwenda kwenye bonanza la mpira la ofisin kwao au lolote ambalo wameplan kwenda na rafiki zake akae nyumban? Aache kwenda shamba kuangalia project zinaendaje akae nyumbani? Sio wote wapo hivyo...wengine ukiwafanyia hivyo watajiona wafungwa.....
 
Kuna wanaume kama vile wamelogwa hata umfanyie nini haridhiki labda aamue kubadilika mwenyewe.
Unaandaa supu akishashiba tu anasepa hapo ndo utajua kweli kunguru hafigiki.
Usawa huu sidhani kama kuna watu weekend wanapumzika zaidi inakuwa siku ya kutembelea vimradi vyake.
 
Back
Top Bottom