Jinsi ya kuishi na mwenye hiv | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kuishi na mwenye hiv

Discussion in 'JF Doctor' started by Zheneba, Jan 21, 2012.

1. Zheneba

Zheneba Member

#1
Jan 21, 2012
Joined: Aug 5, 2011
Messages: 71
Likes Received: 5
Trophy Points: 15
Jaman ndugu yang ameathirika, naomba ushauri ili nisiambukizwe jins ya kuish nae na pia vyakula gan vina mfaa.

2. Preta

Preta JF-Expert Member

#2
Jan 21, 2012
Joined: Nov 28, 2009
Messages: 24,113
Likes Received: 3,033
Trophy Points: 280
dah....mpe pole na umwambie sio mwisho wa maisha....
ukimwi unaambukizwa kwa damu ya mgonjwa au majimaji ya kidonda kuingia kwenye sehemu iliyo wazi ya mwili wako (open cuts)...
sijui utakuwa umeridhika na jibu langu.....na pia elimu ya ukimwi ni pana sana na haupo hivyo unavyoufikiria wewe....

3. n

ngwana ongwa doi Member

#3
Jan 21, 2012
Joined: Dec 26, 2011
Messages: 75
Likes Received: 1
Trophy Points: 0
Pole sana kwamba ufanyaje usiambukizwe njia ambazo HIV huambukizwa ni kwa tendo la ndoa bila kutumia kinga,kuongezewa damu ya mtu mwenye vidudu vya ukimwi,kuchangia sindano,nyembe nk,kugusa damu,majimaji ya mgojwa wa ukimwi kama una mchubuko au kidonda(yaani contact ya damu yako na ya mgonjwa),mama kuambukiza mtoto wakati wa mimba/wakati wa kujifungua.

ufanyaje.
kama wewe ndo huwa unamfulia nguo uwe unavaa glove sababu nguo zaweza kuwa na damu au majimaji usigundue na wewe ukawa na mchubuko mikononi bila kujua ukaambukizwa.

Usichangie vyitu nilivyotaja kama nyembe,sindano nk.

kumbuka ukimwi hauambukizwi kwa kukumbatiana,kucheza pamoja,kushikana mikono,kula pamoja wala hauambukizwi kwa njia ya hewa mfano mgonjwa akikohoa nk.

Lakini ni muhimu zaidi kumuonyesha upendo wa hali ya juu na kumtia moyo na usijionyeshe sana kuwa unaishi naye kwa tahadhari sana ya kuogopa atakuambukiza.

Atumie vyakula kama nyama,matunda kwa wingi,mboga za majani,ndizi,maharage na vyakula vingine vya kumsaidia kujenga mwili.
Usiache kumpeleka kwenye clinic ya wagonjwa wa ukimwi/hosp. huko atapewa msaada zaidi.

4. DAWA YA SIKIO

DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

#4
Jan 21, 2012
Joined: Dec 8, 2011
Messages: 985
Likes Received: 9
Trophy Points: 35

Fine! Zingatia hayo mkuu mleta uzi.
Kuongezea tu kama una uwezo wa kupata antiseptic km savlon,dettol,chlorine etc ni vizuri kuziloweka nguo kwenye maji yenye dawa hizo kwa dak 15- 20 kabla ya kuzifua ukiwa umevaa glavu. Ukikosa basi angalau loweka kwenye sabuni ya unga kwa muda huo.

Loading...