Jinsi ya kufungua simu inayotumia Android Os iliyofungiwa kwenye mtandao mmoja.

Ramlis

JF-Expert Member
Aug 22, 2013
602
519
Kuna njia mbalimbali zinazotumika kufungua simu zinazotumia mtandao mmoja. Hapa tutatumia njia 2.

Njia no 1:
Maandalizi
1/ Kompyuta
2/ Simu iliyofungiwa
3/ Simu inayofanana na hiyo iliyofungwa(Kama iliyofungwa ni Huawei Y330 basi tafuta nyingine ya Huawei Y330 iliyofunguliwa) kama hauna simu download faili linaloendana na simu yako lakni hakikisha lisiwe la mtandao wowote.
4/ Program ya adb
5/ Driver za simu yako
6/ usb cable nzima

Install program ya adb kwenye kompyuta yako, kama una program ya adb.exe uki-install utaikuta kwenye local C: kama una folder la adb liweke mahali popote hata kwenye desktop.
Install driver za simu yako. Baada ya hatua hizo backup stock rom ya simu yako kama tahadhali, kama una simu ya pili backup partition ya system, kama ume-download lifungue file (extract) angalia kwenye file hilo kama lina sytem.img au .bin pia unaweza kukuta folder la system (Kama hautapata file la system fuata njia ya pili). Pia kuna njia ya ku-convert folder la system kwenda .img hii sitaizungumzia kwa leo. kama utapata Systen.img.ext4 futa hiyo .ext4 ibaki System.img au kama ni system.bin futa .bin adika .img

File lako kama tayari unalo la system.img liweke ndani ya folder la adb. Kwenye simu yako iliyofungwa wezesha "usb debug" kwenye developer options. Unganisha simu yako na kompyuta kwa njia ya usb, fungua folder la adb. Ndani ya folder hilo shikilia batani ya shift huku uki-right click mouse baada ya right click achia, utaona sehemu imeandikwa "Open command window here" bonyeza hapo.

Kama folder lako liko local C itafunguka ikiwa imeandikwa hivi C:\adb> kama lipo kwenye desktop itaandika hivi C:\Users\Jina unalotumia\Desktop\adb>.
Mbele ya adb> andika hivi "adb devices" bonyeza enter kwenye keyboard ilikuona kama simu yako inamawasiliano na kompyuta yako angalia kwenye simu yako kama itakuomba kuikubalia au kukataa kuunganishwa ikileta hivyo ikubalie.
Ukifakiwa kwenye cmd ya adb itaonyesha serial number ya simu yako mbele yako itaishia na neno devices. Baada ya hapo andika tena "adb reboot fastboot" bonyeza enter, simu yako itazimika halafu itawakia kwenye fastboot. Kama itashindwa kwenda kwenye fastboot andika hivi "adb reboot bootloader" bonyeza enter.

Ukifanikisha ku-boot kwenye fastboot andika hivi "fastboot flash system sytem.img" bonyeza enter. Hakikisha file la system.img liko ndani ya folder la adb. Itaanza kuhesabu kwa asilimia, ikimaliza itaandika done. kutoka kwenye fastboot andika tena "fastboot reboot' bonyeza enter.

Njia ya pili.

Hapa inahitajika kuwa na simu mbili, moja ya mtandao nyingine ya mitandao yote. Root simu zote halafu flash custom recovery za aina moja simu zote, mfano kama umeweka cwm recovery simu ya kwanza na ya pili pia uweke hio. Chukua simu ya mitandao yote weka memory card kuanzia 4GB na kuendelea, reboot kwenye custom recovery halafu backup rom. ikimaliza toa memory card hamishia kwenye simu ya mtandao mmoja. Reboot kwenye custom recovery, ukiwa kwenye custom recovery format system, ikimaliza ku-format nenda kwenye restore/backup and restore (inategemeana na recovery unayotumia) halafu restore system pekee, ikimaliza fanya factory reset halafu iwashe simu yako.

Mwisho:
Kabla haujafanya lolote kwenye simu yako hakikisha bootloader ya simu yako imefunguliwa. Pia njia hii hutumika kwa simu zenye virus kwa kuflash system pekee.
 
Una-unlock hiyo bootloader kwanza.
Una unlock vipi bootloader? Na je hizi njia zinaweza tumika kuflash huawei smartphone ambazo "emmc is read only?" mfano y300 au y330 kila ukitaka ku update inatoa hiyo message
 
Bootloader ni nin mkuu??
Bootloader ni mfumo unaowekwa kwenye simu ili kuiongoza pale unapoiwasha ndio ya kwanza ku-run. Imewekwa kama security check point kabla simu yako haijawaka. Kwa hiyo kabla haujaifanyia simu yako mabadiliko yoyote ya mfumo endeshi (os) inabidi uifungue bootloader ili iruhusu kufanya chochote unachotaka kinachohusu os.
 
Una unlock vipi bootloader? Na je hizi njia zinaweza tumika kuflash huawei smartphone ambazo "emmc is read only?" mfano y300 au y330 kila ukitaka ku update inatoa hiyo message
Kuna njia mbalimbali ya kufungua bootloader kulingana na simu yenyewe. Kama unatumia android os kuanzia 5 na kuendelea baadhi ya simu ukiingia kwenye developer options utaona sehemu imeandikwa OEM Unlock, kama ipo iweke on.

Baada ya hapo boot simu yako kwenye bootloader, fungua adb andika command kama hivi "fastboot oem unlock" au "fastboot unlock bootloader" kama simu yako italeta maelezo yasome vizuri itakwambia ubonyeze volume up ku-unlock. Kama itakubali itakuandikia pass, kama itagoma tafuta njia iliyo sahihi kwa simu yako.

Simu ikiandika emmc ready only ni kwamba haina uwezo wa ku-write chochote kile. Emmc ndio storage ya simu yenye uwezo wa kutunza kumbukumbu ya kila kitu unachokifanya kwenye simu yako. Ni kama hdd ya kompyuta, kutatua tatizo hilo ni kubadilisha hiyo emmc.
 
Hivi, naweza kuinstall Stock rom ya Tecno y3 kwenye Tecno y3+?? Lengo kuunlock sim
 
Hivi, naweza kuinstall Stock rom ya Tecno y3 kwenye Tecno y3+?? Lengo kuunlock sim
Ndio unaweza lakni ni system tu, lakni kulingana na matumizi huko mbeleni kuna mapungufu utayaona kwenye simu yako. Mimi nilijaribu kubadili kwenye simu ya rafiki yangu ikakubali ndo nasubiria mrejesho kutoka kwake. Mwanzoni nilimuwekea la y2 alitumia vizuri tatizo lilikuwa kwenye sauti ndo nikaweka la y3.
 
Back
Top Bottom