Jinsi ya kufanya kazi na Boss mkorofi na kuepuka mikwaruzano

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,896
36,215
Habari zenu za asubuhi ndugu wapendwa.
Ni siku nyingine tulivu ambayo mwenyezi ametuteua kati ya wale wengi kuwa tunafaa kuendelea kuvuta pumzi hii ni jambo la kushukuru maana kama tungepata kuona ni jinsi wengi wameikosa nafasi hii ili hali wanaitaka
sote tuseme AMEN.....

Bila ya shaka makazini ndio sehemu tunapotumia muda mwingi sana kwani ndio sehemu tunapopata mkate wetu wa kila sikukazini ni mahali ambapo wakati mwingine panakuwa na changamoto nyingi na hata wakati mwingine ufikiria kuachana na kazi hiyo na kutafuta pahali pengine changamoto kubwa ninayoitaka kuizungumzia hapa ni ukorofi wa wakuu wetu wa kazi (ma BOSS) wakati mwingine mkuu wa kazi anaweza kukufanya kazi uione chungu.

Zifuatazo ni njia zinazoweza kusaidia kukabiliana na changamoto hizo..

1)- Fika katika eneo lako la kazi kwa wakati uliowekwa na ofisi.

Mara nyingi mkuu wako wa kazi malalamiko yake huwa kuna chanzo.
Unaweza wewe usione chanzo lakini kwa uzoefu wangu ni kwamba ugomvi mwingi wa mfanya kazi na mkuu wa kazi ni mfanya kazi kuchelewa kuingia kwenye eneo lake la kazi. Kampuni imenunua muda wako wa kukaa hapo na kufanya kazi kwa malipo ya kwa mwezi , wiki au siku.

Kitendo cha wewe kuchelewa kuingia kwenye eneo lako la kazi ni kama unamuibia muda ambao yeye anakulipa kwa kuwa pale.....hivyo lazima boss awe mkali kwako.....

2)- Fanya kazi unazopewa kwa wakati

Upo hapo kwa ajili ya kazi na unalipwa kwaajili hiyo kwa hiyo kwanini ulazimishwe kufanya kitu unacholipwa? Unapotimiza wajibu wako unamfanya boss wako akuheshimu....na akose sababu ya kukulamikia bila ya sababu.

3)- Kubali makosa.

Wakati mwingine malalamiko ya wakuu wa kazu yanatokana makosa yetu ya kiutendaji. Kwahiyo unapokubali kosa ni kwamba unakubali kuwa ulijikwaa na maana umeshajua kosa lako na hutarudia tena na huo ndio ukomavu unaotakiwa kuwa nao kwenye sehemu za kazi za watu wengi.

4)- Mpe heshima yake.

Kumpa heshima yake sio kumsujudia bali ni kufuata malekezo na taratibu za kazi anazokupa kwa wakati kwani hata yeye anawajibika kwa watu wa juu yake kwa makosa ya kazi alizokupa.

5)- Epuka ukaribu uliopitiliza


Kuwa karibu na mtu ni jambo zuri lakini inategemea na huyo mtu huo ukaribu anauchukuliaje kwa wakuu wa kazi ukaribu ni kama kumzoea na kuharibu kazi.....

6)- Heshimu muda wa kazi.

Nina hakika kila sehemu pana taratibu zake muda wa kazi na muda wa mapumziko ikiwa ni muda wa kazi basi fanya kazi na ionekane kuwa ni kazi kweli.


Nawasilisha
 
Akiwa na roho ya korosho,hata kipindi cha mvua,atasema unamtimulia vumbi.

Wengi wao ukorofi ni kutokana na kutojiamini,akihisi utampoka nafasi yake.

Alaf wanakuwaga wachawi haooo,unafikiri mchawi anamuamana na mtu?????
 
Hizo ulizozitaja mbona ni taratibu za kawaida sana za ku-behave ukiwa chini ya Boss yeyote yule, awe mpole au mkali.

yaani kama hizi;
>Fika katika eneo lako la kazi kwa wakati uliowekwa na ofisi.....
>Fanya kazi unazopewa kwa wakati
>Mpe heshima yake.....
>Heshimu muda wa kazi......

hizi ni taratibu unazopewa mapema kabisa unapoanza kazi huenda hata kabla hujamjua bosi wako..!

Haya mambo mengine kama kuepuka ukaribu uliopitiliza na kubali makosa.... haya hupewi na ofisi lakini ni mambo ambayo unatakiwa uwe umejifunza kutoka tangu huko ulipotoka kwa mfano kipindi upo shuleni, ni mambo ambayo unatakiwa u-behave kwa waalimu wako. Na hata kama upo kwenye ajira wala haihitaji uyafanye eti kwa kuwa upo na boss mkali au mpole!

Mi naona suala la kumkabili boss mkorofi lipo variable sana na halina kanuni maalum, hii inatokana na wewe mwenyewe uzembe wako ukoje na boss wako ana ukorofi wa aina gani na kwa kiasi gani.
Ukijua hayo ndio utaweza kumshauri mtu jinsi ya kuishi na huyo boss wake kulingana na namna tatizo lilivyokaa..!

BTW, kutoa ushauri ni kipaji na pia ni taaluma maalumu, maana kila tatizo linakuja na umbo lake tofauti.
 
Maelezo mazuri lkn ukorofi wa mabosi unatofautianaa..... Kuna wengine wanawachapa makofi wafanyakazi wa chini basi tuu kuwaonea
 
Mkuu natimiza wajibu wangu vizuri kabisa..Sema visa haviishi kila uchwao
Angalia sheria zinasemaje za hapo kazini kwako.Kuna mabosi huwa wakorofi tu anza kutumia taratibu za kisheria kumshughulikia kisheria kwa mamlaka husika ziwe za ofisini nk
 
Natumaini wengi tumejifunza kuna tabia ya kulalamika Bosi Mkorofi kumbe chanzo ni wewe mwenyewe.
Somo zuri sana. Ngoja nisave!
 
Back
Top Bottom