Jinsi ya kuendesha Ngalawa

kwangu na kwako ila kwao ni salama tu



kuogelea naogeleaga coco ila kinachowaua watu baharini sio kutojua kuogelea bali kuchoka na baridi

si unaogelea uku umevaa jaketi la baridi kabisa
 

Hahahahaaaaa! Yalinikuta hayonilipotembelea watu wangu kijiji fulani when I finished my exam (A level)

Nilipenda siku moja niwafate kuvua coz kuna madogo tu walikua wanakwenda, nakumbuka wazee walinisisistiza nisiende coz wimbi kali na kutapika ningerudi mgonjwa. Nilipenda kuona namna watu wanavyovua huku nikijisemea nitajifunza mengi.

Siku nikakomaa nakuwafata.
Mwanzoni safari ilikua tamuu, coz tulikua ktk mto (pwani) = tulikua tunapita pwani/mto ulioga vitongoji viwili. wataki tunaingia baharini ndio kasheshe! coz mbele yetu kulikua na kisiwa, mean mbele kutakua na sehemu mbili za kuingia bahari kuu (wanaita milango) Dah aliekufa Mungu amrehemu! Mawimbi ya bahari kuu yanapiga kwa kasi milangoni.

Kabla ya kuvuka hapo, nilijua ni kazi nyepesi sana kuvuka kwani nilipoona weupe kwa mbali nilijua ni vijiwimbi vidogo vidogo tu!!! Kuyakaribia nilistka sana na kujisemea pale tunazama, kudadadeki wimbi linakingoe nasi ndio tunatakiwa kuyafesi kwa mbele, coz ukiyapa ubavu chonbo kinapinduliwa! niliamua kutoangalia mbele thus nikagekia tulipotoka, ile tunaanza kuyakata, maji yameshaanza kuingia kwenye chombo! Nikapewa kazi ya kutoa maji, yule mmoja kasimama kwenye behewa kukibalance chombo kutokana na mawimbi na upepo na mwengine alikua ndie dereva anadeal na usukani wake (tanga). Tulikua watatu.

Wakati natoa maji nilijaribu kuangalia mbele, hapo ndipo nilipobugi! coz ilikua ni kati kati ya mlango kuingia main sea. ile nageuka tu wimbi kubwa inakuja na ilikua na kimo cha mtu mzima kabisa! wakati naishangaa ndio inatpita sasa!! kudadadeki kidoo kilitupwa kule, tuliloa hadi nywele! nilishikwa na mfadhaiko na kujua leo kifo tu. Kwa bahati vidoo vilikua viwili nilikaripiwa kutoshangaa na niendelee kutoa maji. kile kidoo kilichoondoka na maji nikaambiwa hakiwezi fatwa coz chombo hakitakiwi kugeuza mbavu pale.

Tuliingia bahari kuu ambapo hakuna mawimbi ya kutembea ila ni maji kujifinya kwa chini na kurudi juu mwanzo mwisho, yaani kama upo kwenye bembea vile!!! na hali hiyo ndio huwafanya wengi kutapika (wageni)

Nashukuru tulirudi salama. Ila sitakaa niisahau kamwe siku hiyo.
 
Nawaonaga pale ferry wana endesha na mwiko, dereva anaendesha utadhani anasonga ugali. Mwambie kama anajua kusonga ugali anaweza akaendesha hicho kiboti ngalawa.
 
Nawaonaga pale ferry wana endesha na mwiko, dereva anaendesha utadhani anasonga ugali. Mwambie kama anajua kusonga ugali anaweza akaendesha hicho kiboti ngalawa.

daaaaaa! nimecheka hatari so ukijua kusonga ugali basi unaendesha dah! kwa hiyo mamantilie wasonga ugali wanaweza sio
 

Mashaxizoumetisha
 
Last edited by a moderator:
Hii kitu sitaki hata kuisikia! kwenda kutongoza samaki! yalinikuta miaka ya 80hapana hicho chombo mpaka ujifyatue akili kidogo ndo ukipande oh hapana! unaliona wimbi kubwa kama ppf tower kisha linawapiga mnaenda juu nikajua leo sijui but kwa kudra ya mwenyezimungu tulifika ila jasho lilinitoka.
 

Kiongozi, simulizi nzuri sana, asante ku share nasi!!!
 
unaogopa sana, wenyewe wanaiamini ngalawa kuliko hata meli, na wana sababu zao
1 ngalawa haizami, ikizama waibirua na kufata maji
2 ngalawa una uwezo wa kufunga breki na ukasimama hapo hapo
3 kama utakuwepo upepo, basi ngalawa ina spidi kuliko boti
twayyib!! Akhii hivi ni wapi wanatoa kozi ya kuendesha boti Ndogo (out engines)? kwa dar es salaam au zinjibar?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…