Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,569
- 9,429
JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA DENGU ZA NAZI NA VIAZI .
Vipimo:
1. Dengu zilopasuliwa 2 vikombe
2. Viazi 3
3. Kitunguu 1
4. Nyanya 1
5. Pilipili mbichi na thomu iliyosagwa 1 kijiko cha chai
6. Methi (uwatu) uliosagwa 1/2 kijiko cha chai
7. Majani ya mchuzi (curry leaves) kiasi 5
8. Haldi (bizari ya manjano) 1/2 kijiko cha chai
9. Kotmiri (giligilani) iliyokatwa katwa 1
10. Msongo (bunch) Ndimu 1
11. Chumvi kiasi
12. Tui la nazi 1 kikombe
13. Mafuta 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Roweka dengu kwa muda wa masaa, kisha zichemshe ziwive. Maji tia kiasi tu ili zibakie dengu na supu kidogo tu.
2. Karibu na kuiva tia viazi vilivyomenywa na kukatwakatwa vidogo vidogo. Katakata kitunguu na nyanya, weka kando.
3. Weka mafuta katika sufuria ya kiasi, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi. Tia majani ya mchuzi kaanga kidogo, tia methi (uwatu), kisha tia thomu na pilipili, nyanya na bizari ya manjano. Mimina dengu na viazi vyake kisha tia ndimu, chumvi.
Tia tui la nazi na uache kidogo ichemke, Tia kotmiri iliyokatwakatwa ikiwa tayari.