Jinsi wazungu, wahindi na wachina wanavyokuja Bongo mikono mitupu na kuondoka na mamillioni

Magnificient

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
1,162
701
Kwanza kabisa nianze kwa kupongeza mfumo wa maisha na utaratibu wa wenzetu hususan watu wa Ulaya, Marekani, China na India kuweza kuanzisha, kusimamia na kuendeleza biashara za ndani na nje ya nchi zao na kuweza kumiliki biashara popote duniani. Mfumo wao na mazingira yao husaidia sana kuchochea ubunifu na uzalishaji mali ndani na nje ya nchi zao.
investor.jpg

Mambo matatu ambayo hutayakosa katika biashara zao ni ujuzi (skills), uzoefu (experience) na mtandao (network). Na hufanikisha hilo kwa kuzingatia kufanya kazi kama timu (team work). Mambo mengine yote ambayo unayajua ni muhimu kwa mafanikio ya biashara hufuata baada ya hayo – mtaji, soko, elimu, miundo mbinu nk.
Hii imewasaidia sana kufanikiwa katika mengi kati ya yale ambayo wanayagusa (kuna machache pia wanafeli na biashara zao hufa kama hawaida).
Sasa ukija kwa hawa wazungu, wamarekani, wachina na wahindi wanaokuja bongo “kutazama mazingira” utakuta kuna wale ambao tayari wana mitaji (Ila kwa kuanzia wanakuja mikono tupu pesa wakiwa mameziacha kwao) na wale ambao wanakuja wakiwa hawana mitaji, ila akili nyingi sana kichwani na umafia kiasi fulani mkononi. Si unajua kwamba biashara ni bahati nasibu na ni mashindano pia?
Achana na hao wenye mitaji na angalia hawa ambao wanakuja mikono tupu na huko kwao hawajaacha kitu. Wanakuja bongo na kutazama sekta za afya, ujenzi, hoteli, uchukuzi, viwanda, tehama (ICT) na kadhalika kisha wanakusanya kila taarifa ya muhimu, kuzichambua taarifa hizo na kupata picha HALISI ya soko la bongo. Baada ya hapo “the rest is history”.
avic town.jpg

Wanatumia ujuzi, uzoefu na mtandao walionao kujua, kuanzisha, kusimamia na kuendeleza biashara kubwa ambayo uwezekano wa kufaulu ni mkubwa zaidi kwa kuwa imejengwa katika msingi mzuri na imara. Utafiti ulifanyika, taarifa zilichambuliwa, hitaji likajulikana, changamoto zikajulikana, faida ikaonekana, athari za serikali zikaonekana, ramani ikachorwa na uwezekano mkubwa wa kutoka “point A” kwenda “point B” ukahakikishwa.
Baada ya hapo wanaratibu (organize) na serikali, ndugu, jamaa, marafiki, wawekezaji, wafanyabiashara na kadhalika wanachangia nguvu – mtaji, utaalam, uzoefu, mtandao nk na kupata nguvu kubwa zaidi hata kama wapo ugenini. Pia mfumo wao unawapa fursa ya kukuza mtaji kwa urahisi na kusaidiwa popote watakapokwama, kwa hiyo biashara ya mtu mmoja inasaidiwa na vitu vingi sana.
Kwa njia hiyo hata mzungu au muhindi akija mikono mitupu baada ya muda atakuwa na mamillioni kwa mamillioni. Hivyo ndo jinsi ambavyo wageni wanatawala soko la biashara nyumbani kwetu na sisi wenyeji tuliowengi tukibaki kuwa wateja na wafanyabiashara wadogo wadogo.
Angalia makampuni makubwa ya dawa, madini, uwindaji, hospitali, hoteli, viwanda, malls, mawasiliano, real estate (sijui kwa Kiswahili inaitwaje), teknolojia, nishati, simu na kadhalika ya hapa bongo yanamilikiwa na nani? Wapo wangapi? Jibu utakalopata ni “wageni” na “wapo wengi” ndani ya kampuni moja, kila mtu kachangia chake.


Hivyo ndivyo ilivyo, na hivyo ndivyo wanavyokuja mikono tupu ila uwezo wa kuratibu (organize), akili nyingi kichwani na ujanjaujanja mwingi na kufanikiwa kuondoka na mamillioni. Hakuna kubebwa wala siri, ni kuwa wazuri tu katika kunusa fursa na kuratibu jinsi ya kushinda fursa hizo.

Sasa mimi na wewe mbongo mwenzangu tunafanyeje – tufanye kama wao au tukaombe kazi kwenye miradi yao?

Siku njema!


msaada.jpg
 
Back
Top Bottom