Jinsi wanasiasa wanavyoharibu elimu hapa nchini

thereitis

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
297
41
Tumeshuhudia matokeo mabovu ya kidato cha nne miaka miwili mfululizo, 2010 na 2011. Haya ni matokeo ya siasa uchwara katika mipango ya elimu. Ni wanasiasa wanaoshawishi au kulazimisha mipango mingi ya elimu hapa nchini. wataalam wa sekta ya elimu wamekuwa wakitekeleza matakwa ya siasa ili kunusuru ajira zao. Mfano mmojawapo ni uanzishwaji wa shule za kata mwaka 2006 chini ya uongozi wa waziri mkuu aliyejiuzulu; shule nyingi za kata zilianzishwa bila kujali ubora wa elimu.

Wanasiasa wamekuwa wakiwadanganya wananchi kwa kutumia takwimu ya wanaohudhuria shule na siyo ubora wa elimu. Swali kwa wanajamii wenzangu ni Je, ni jinsi gani wanasiasa wanachangia kuharibu au kuboresha mipango ya elimu hapa nchini? Mimi nimetoa mfano mmoja wa shule za kata.
 
Mikopo ya elimu ya juu: serikali inawalipia wanaosoma ualimu wa masomo ya sayansi 100 perce. Masomo mengine wanafunzi wajilipie wenyewe. Hii maana yake nini?
1. Watoto wa wakulima hawatakaa wasome masomo ya kujilipia kama sheria, uchumi na biashara.
2. Watoto wa wakulima watabaki kuwa waalimu wa sayansi tu. na sayansi yenyewe haina mazingira mazuri.
3. wenye hela watasoma masomo yanayowapelekea kuwa watawala.
 
Jamani mimi sijapost hizo comment za kipuuzi hapo juu kwani kuna gamba katumia kupost huo ujinga bkzo nilicuwa sija-rogout.
 
Shule za kata zinaimprove kadiri siku zinavyoenda, hizo ni propaganda za wamiliki wa shule binafsi na wamiliki wa shule za kidini, baada ya kuona wanakosa watoto wa kusoma shule zao.
Usikubali kupelekwa pelekwa kiasi hicho kaka.
Mimi naunga mkono kweli kuwa wanasiasa wanaharibu elimu hasa elimu ya juu, wanafunzi wanashiriki siasa na wanakuwa na uwezo mdogo madarasani.
 
Shule za kata zinaimprove kadiri siku zinavyoenda, hizo ni propaganda za wamiliki wa shule binafsi na wamiliki wa shule za kidini, baada ya kuona wanakosa watoto wa kusoma shule zao.
Usikubali kupelekwa pelekwa kiasi hicho kaka.
Mimi naunga mkono kweli kuwa wanasiasa wanaharibu elimu hasa elimu ya juu, wanafunzi wanashiriki siasa na wanakuwa na uwezo mdogo madarasani.

Takwimu alizotoa zinahusu shule za kata,ina maana na hawa wanashiriki siasa?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Ama hakika elimu yetu imekuwa ni bora elimu tu na sio elimu bora tangu shule za kata zianzishwe, mi naona shule za kata zimekuwa ni vijiwe tu vya wavuta bang na kuandaa vimalaya. mfano ni saa 3 asubuh muda wa darasan kabsa wavikuta vitoto vichakan n "no body cares at all" ni nini hiyo mwadhan?
 
Back
Top Bottom