Jinsi tunavyozidi kujidharirisha

Jinsi tunavyozidi kujidharirisha

fahad_salum

Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
22
Reaction score
25
Moja kati ya faida kubwa ambayo CCM inajivunia basi ni kuwa na Taifa lenye ujinga mwingi, watu ambao sio wasomi na umaskini

TAIFA LA WAJINGA
Hapa nasema kwa kuangalia idadi kubwa ya raia hasa kwenye vijiji vya ndani ndani.Nchi ya ahadi hii, ukitaka cheo basi toa ahadi ambayo hatakama huwezi ukaitatua watu watakuchagua.Nashukuru mungu mambo yameanza kubadilika kabisa,watu wameanza kwenda shule lakini tatizo bado lipo kwenye kushadidia Ahadi zisizo na msingi

Kwa taifa kama Tanzania ahadi wananchi tushazichoka tunasubiria vitendo tu.Kwanini ziwe ahadi? Mpaka lini? Kwanini usiwe vitendo?

1: Tumeahidiwa Mil 50 kila kijiji ziko wapi? Kwanini utoe ahadi wakati huwezi ukaifanikisha? Tumechoka N ahadi

2: Viwanda vimejengwa vingapi?
Kwanini ahadi? Ifike stage kila kiongozi anayetaka kupata Cheo basi atoe hoja za kivipi tunaweza tatua changamoto tulizonanazo lakini si ahadi tumechoka

TAIFA MASKINI
Tupo dunia ya 3 kiuchumi. Wananchi wengi wanaishi kwa kutumia chini ya dola kwa siku huu ni umaskini mkubwa.Nasema umaskini unahusika kwa sababu wananchi wengi huishia kupewa kanga za bure, kofia, mashati ya bure na kugawa kura bila haki.Tunadidimia

Tanzania yangu inakila madini, vyanzo vya maji, mbuga za Wanyamapori kwanini bado tupo nyuma hivi?

Kwanini tupo nyuma? Kwanini isiwe ahadi iwe vitendo tu? Hivi ni wapi tumeshindwa? Au ni wapi tumekosea?

Viongozi wanabidi waje na hoja madhubuti ili kuleta mikakati bora ya maendeleo yetu lakini si ahadi tena.Tukiendelea na ahadi tutabaki miaka yote nyuma pasipo kupiga hatua yoyote kwenda mbele.

Kuna sehemu tumekosea in fact tunajidharirisha watanzania.Tuna mali zote hizi bado tupo nyuma tu tunajidharirisha

Usinambie Tanzania tuna maadui kumi wakati tuna maadui wa tatu tu
Umaskini
Ujinga
Maradhi
bb184c680c12c73d29bc7c43f89a0afa.jpg
 
Mkuuu Tanzania kinacho sumbua ni ujinga na umaskini.Haiwezekani kila baada ya miaka mitano tunadanganwya lakini tunazdi kuwashangilia na kuona hakuna wakombzi tofauti na hawa watu wa Lumumba
 
Tunafanana na nchi karibu zote Africa ukiondoa Azania (South Africa) so maendeleo yataenda hatua kwa hatua kadri siku zinavyokwenda na population kuongezeka pia.ni kama mtoto anavyokua toka chini kwenda ukubwani.na hiyo haitakaa ikapingika hata tukikuweka wewe uongoze nchi,makosa kadhaa hayaepukiki na yanapotokea hurekebishwa taratibu mpaka tutafika tu.miaka mingine 50 mbele hatutakua hivi hata kidogo,sasa mtu asidhanie mafanikio ya nchi na wananchi ni kama kufungua bomba na yatokee tu ghafla kipindi na yeye akiwa anaishi hapa duniani.inawezekana maendeleo makubwa yakaikuta nchi yetu tukiwa tulishalala makaburini,ni swala la wakati tu,narudia tena hata umuweke nani mamlakani maendeleo ni kama kupanda ngazi,moja baada ya nyingine na maneno mengine mengi ni mbwembwe tu na lawama zisizo na maana

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Ni hivi tukirudi nyuma 1961 Tanzania na nchi zinazojulikana Tiger countries ambazo ni China, Malaysia, Singapore....etc tulikuwa sawa kiuchumi na tulikuwa na ushrikiano mzuri tangu kipindi hicho hadi hivi sasa. Ila ukiangalia kiuchumi hivi sasa yaani wametuacha pa kubwa! Lazima tujifunze nini wenzetu walifanya hadi wakapiga hatua kutuzidi sisi na siyo kuhangaika na wapinzani wakati watu wanataka maendeleo kuna watu wanathubutu kuwekeza nguvu, muda, na fedha kwaajili ya kupambana na vyama vya upinzani ambao ni watanzania wenzake badala ya kupambana na shughuli za maendeleo kwaajili ya watanzania.
Ni naamini, ukifanya jambo zuri kwa manufaa ya walio wengi/taifa kwa ujumla wake ni lazima utapongezwa tu na kupewa sifa stahiki na siyo kulazimisha sifa. Kama mpaka leo bado tunasumbuliwa na ujinga, maradhi, na umaskini ni nani tunamsubiri aje amalize hayo matatizo? Halafu kwa nchi hii ujinga ndiyo unaongoza na ndiyo unachangia kila kitu kisiwe na tija kama tunavyopenda iwe.
 
Umekosea kidogo, si Ccm pekee inayojivunia bali vyama vyote vya siasa vinajivunia kuwa na wajinga wengi, hivi sakata la Lipumba na CUF, matibabu ya Lisu na maandamano yasiyo na tija, kama si ujinga wa watanzania hivi unafikiri kuna mtu angevielewa hivi vyama vya siasa vya bongo?
 
Tatizo ni kwamba polojo ni nyingi kuliko vitendo ingefaa sana tukampata kiongozi wa vitendo hata katka mikutano asipoongea sana watu wakapiga makofi na kumshangilia lakini tukaona vitendo
 
Tunafanana na nchi karibu zote Africa ukiondoa Azania (South Africa) so maendeleo yataenda hatua kwa hatua kadri siku zinavyokwenda na population kuongezeka pia.ni kama mtoto anavyokua toka chini kwenda ukubwani.na hiyo haitakaa ikapingika hata tukikuweka wewe uongoze nchi,makosa kadhaa hayaepukiki na yanapotokea hurekebishwa taratibu mpaka tutafika tu.miaka mingine 50 mbele hatutakua hivi hata kidogo,sasa mtu asidhanie mafanikio ya nchi na wananchi ni kama kufungua bomba na yatokee tu ghafla kipindi na yeye akiwa anaishi hapa duniani.inawezekana maendeleo makubwa yakaikuta nchi yetu tukiwa tulishalala makaburini,ni swala la wakati tu,narudia tena hata umuweke nani mamlakani maendeleo ni kama kupanda ngazi,moja baada ya nyingine na maneno mengine mengi ni mbwembwe tu na lawama zisizo na maana

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
Mkuu nitofautiane na wewe kimtazamo
Inchi nyingi za kiafrica hazina viongozi walio kwaajiri ya maslahi ya wanainchi, hakuna wazalendo kila mtu yupo sehemu flani kwaajiri ya kutimiza adhima yake wanainchi wengi ni kundi la wajinga waliopitiliza
Africa haitaendelea kamwe labda itawaliwe
 
Tunafanana na nchi karibu zote Africa ukiondoa Azania (South Africa) so maendeleo yataenda hatua kwa hatua kadri siku zinavyokwenda na population kuongezeka pia.ni kama mtoto anavyokua toka chini kwenda ukubwani.na hiyo haitakaa ikapingika hata tukikuweka wewe uongoze nchi,makosa kadhaa hayaepukiki na yanapotokea hurekebishwa taratibu mpaka tutafika tu.miaka mingine 50 mbele hatutakua hivi hata kidogo,sasa mtu asidhanie mafanikio ya nchi na wananchi ni kama kufungua bomba na yatokee tu ghafla kipindi na yeye akiwa anaishi hapa duniani.inawezekana maendeleo makubwa yakaikuta nchi yetu tukiwa tulishalala makaburini,ni swala la wakati tu,narudia tena hata umuweke nani mamlakani maendeleo ni kama kupanda ngazi,moja baada ya nyingine na maneno mengine mengi ni mbwembwe tu na lawama zisizo na maana

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
ACHA KUJAZA WATU UPUPU. LEO MIAKA 50+ YA UHURU WETU UNATULETEA POROJO ZA AKILI ZA KISHAMBA
 
Moja kati ya faida kubwa ambayo CCM inajivunia basi ni kuwa na Taifa lenye ujinga mwingi, watu ambao sio wasomi na umaskini

TAIFA LA WAJINGA
Hapa nasema kwa kuangalia idadi kubwa ya raia hasa kwenye vijiji vya ndani ndani.Nchi ya ahadi hii, ukitaka cheo basi toa ahadi ambayo hatakama huwezi ukaitatua watu watakuchagua.Nashukuru mungu mambo yameanza kubadilika kabisa,watu wameanza kwenda shule lakini tatizo bado lipo kwenye kushadidia Ahadi zisizo na msingi

Kwa taifa kama Tanzania ahadi wananchi tushazichoka tunasubiria vitendo tu.Kwanini ziwe ahadi? Mpaka lini? Kwanini usiwe vitendo?

1:Tumeahidiwa Mil 50 kila kijiji ziko wapi? Kwanini utoe ahadi wakati huwezi ukaifanikisha? Tumechoka N ahadi

2:Viwanda vimejengwa vingapi?
Kwanini ahadi? Ifike stage kila kiongozi anayetaka kupata Cheo basi atoe hoja za kivipi tunaweza tatua changamoto tulizonanazo lakini si ahadi tumechoka

TAIFA MASKINI
Tupo dunia ya 3 kiuchumi. Wananchi wengi wanaishi kwa kutumia chini ya dola kwa siku huu ni umaskini mkubwa.Nasema umaskini unahusika kwa sababu wananchi wengi huishia kupewa kanga za bure, kofia, mashati ya bure na kugawa kura bila haki.Tunadidimia

Tanzania yangu inakila madini, vyanzo vya maji, mbuga za Wanyamapori kwanini bado tupo nyuma hivi?

Kwanini tupo nyuma? Kwanini isiwe ahadi iwe vitendo tu? Hivi ni wapi tumeshindwa? Au ni wapi tumekosea?

Viongozi wanabidi waje na hoja madhubuti ili kuleta mikakati bora ya maendeleo yetu lakini si ahadi tena.Tukiendelea na ahadi tutabaki miaka yote nyuma pasipo kupiga hatua yoyote kwenda mbele.

Kuna sehemu tumekosea in fact tunajidharirisha watanzania.Tuna mali zote hizi bado tupo nyuma tu tunajidharirisha

Usinambie Tanzania tuna maadui kumi wakati tuna maadui wa tatu tu
Umaskini
Ujinga
Maradhi
bb184c680c12c73d29bc7c43f89a0afa.jpg
kaka Fahad umeongea kitu cha maana sana, niliwahi kusafiri na air tanzania miaka ile walipokuwa na ile air bus tuliyoazimishwa na mchina, nilikuwa natokea dar kwenda mwanza, nilikaa na kaka 1 kama shombe la kiarabu lakini anaishi saudia ila mzaliwa wa mwanza, alisema waarabu wana mafuta tu na wametuzidi mbali sana, sisi tuna madini, mbuga za wanyama, tuna kila kitu cha kutufanya tuwe matajiri, lakini bado ni maskini, nikasema ni kweli, tunashindwa hata kupeleka matangazo kwenye mashirika makubwa kama bbc, cnn, aljazeera watangaze utalii, kisa tu mkono mfupi, jamaa alikuwa analalamika sana mie namsikiliza tu, nikamwambia mie na wewe ndugu hatuna sauti, hata tukipaza vipi bado pesa itapigwa kwa individuals lakini sio serikali
 
Akili ndogo hauwez kuongoza akili kubwa. Unazungumzia eti maendleo ni hatua miaka hamsini ya uhuru. Bado tunafundishana uzalendo,,maji ya kunywa hamna, elimu duni, huduma za afya duni,watu wanazid kuwa maskini. NAFIKIRI ULIKUWA UNAZUNGUMZIA HATUA ZA MAENDLEO KURUDI NYUMA. Acheni jokes bhana. Tuache kulishana matango pori. Ayo wape wanao nyumbani.

Sent from my TECNO M5 using JamiiForums mobile app
 
Tunafanana na nchi karibu zote Africa ukiondoa Azania (South Africa) so maendeleo yataenda hatua kwa hatua kadri siku zinavyokwenda na population kuongezeka pia.ni kama mtoto anavyokua toka chini kwenda ukubwani.na hiyo haitakaa ikapingika hata tukikuweka wewe uongoze nchi,makosa kadhaa hayaepukiki na yanapotokea hurekebishwa taratibu mpaka tutafika tu.miaka mingine 50 mbele hatutakua hivi hata kidogo,sasa mtu asidhanie mafanikio ya nchi na wananchi ni kama kufungua bomba na yatokee tu ghafla kipindi na yeye akiwa anaishi hapa duniani.inawezekana maendeleo makubwa yakaikuta nchi yetu tukiwa tulishalala makaburini,ni swala la wakati tu,narudia tena hata umuweke nani mamlakani maendeleo ni kama kupanda ngazi,moja baada ya nyingine na maneno mengine mengi ni mbwembwe tu na lawama zisizo na maana

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
Tangu mia ya 60 tulikuwa hivihivi hata baada ya miaka 60 kupita.
Still unataka miaka 30 mingine?
You can't be serious.
 
Back
Top Bottom