Kaliculus
JF-Expert Member
- Nov 8, 2019
- 271
- 248
This is a true story...
Nakumbuka ilikuwa mwezi wa saba, kipindi ambacho shule zilikuwa zinafunguliwa kwa ajili ya wanafunzi kuendelea na Muhula wa pili wa masomo.
Kipindi hicho niko kidato cha pili, shule X mkoani Tanga, na hii ilikuwa 2004. Shule yetu ilikuwa mbali na mji, kama Kilometa 40 hivi toka Halmashauri ya mji na usafiri wa kwenda na kurudi uliokuwepo kipindi hicho ulikuwa zile kenta ambazo zilikuwa na siti nyuma maarufu 'Chaimaaarage'. Waliokwenda Zanzibar watafahamu maana huko bado zipo.
Basi bwana, usafiri ilikuwa Chaimaarage moja, ila baadae kuna kampuni maarufu ya Handeni huko(wenyeji wataielewa hii kampuni) wakaleta basi kubwa moja, tukashukuru sana. Sasa ikawa ukikosa hilo basi yakulazimu upande Chaimaarage au ulale usafiri siku inayofuata kwani enzi hizo bodaboda bado hazikuwepo.
Nirudi kwenye mada sasa!!!
Siku ya tukio nakumbuka niliwahi mapema kituo cha basi, nikaweka mizigo yangu nikawa nasubiri muda wa safari kuanza.
Kwa vile ilikuwa kipindi cha kufungua shule, kulikuwa pia na idadi kubwa ya wanafunzi wanasafiri kwenda shuleni, na mmoja wao nimwite Pendo(siyo jina lake halisi) tulisoma darasa moja na alikuwa rafiki yangu, tukaonana muda mchache kabla ya safari kuanza, baada ya salam akasema yuko na baba yake hivyo tukamsalimie, hivyo tukaongozana.
Ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona yule mzee na kumbe siku ile ingekuwa mara yetu sote ya mwisho kumuona... Hakuna aijuaye baadae yake.
Muda wa safari kuanza ukafika, nakumbuka gari ilijaza sana siku ile, nadhani ni kwasababu ya shule kufunguliwa, lakini pia kuna wafanyabiashara walikuwa wanatoka gulioni. Ilikuwa siku ya gulio/ mnada pale Korogwe kama sikosei.
Basi bwana, tukaianza safari salama kabisa, japo nilipata siti lakini sikutaka kukaa, kama ujuavyo tulikuwa wanafunzi wengi, zile chereko za kuwa pamoja 'peer groups' nadhani zilitufanya tuone kubanwa/ kukosa uhuru kukaa kwenye siti kuliko kusimama, hivyo tulisimama karibu wote na safari tukaiona nzuri kwa stori za hapa na pale kati yetu.
Sasa basi, barabara ya kwenda shuleni ilikuwa imezunguukwa na misitu na vichaka vingi, yaani ni pori kwa pori na humo njiani ni vijiji vidogo vidogo vya wastani wa nyumba kama tano ( familia moja moja) wakilima na kufuga. Sasa basi tukiwa kaikati ya safari, mara ghafla tukashtukia gari inayumba, halafu ikasimama kwa ghafla. Sasa abiria wakawa wanapiga kelele sana, hatukuelewa ni kitu gani kinatokea.
Mara tukaona watu wamefunika nyuso zao kwa vitambaa'mask' wanavunja vioo na mlango (ulifungwa) kwa kasi kubwa kwa kutumia mapanga na marungu, nadhani ilikuwa kututisha. Wakafanikiwa kutuliza watu, pakawa kimya kabisa, basi wakatuamuru tushuke garini mmoja mmoja, na ukiteremka ukifika chini tuu unaamriwa kuvua nguo zote halafu unalala chini kifudi fudi. Aisee tuliadhirika sana siku ile. Wakati niko chini pale nimelala miongoni mwa wasafiri wengine, nikasikia mlio wa bunduki, sikujua ni kwaajili gani.
Basi walipoondoka tukaanza kutafuta nguo tujistiri, na ndo hapo tukapata taarifa kuwa yule mzee (baba yake Pendo) ameuawa kwa risasi na wale majambazi( ule mlio wa bunduki). Kuna wanaosema sababu ni kukataa kuvua nguo, maana alikuwa na mwanae mle garini na wengine wakadai alimfahamu jambazi mmoja kwa sauti na akamwambia, " fulani hata wewe umo?", ila ndo hivyo alishakufa.
Sasa basi, baada ya purukushani ile na akili kukaa sawa, mara najiona nimelowa damu suruali haifai, ndo kujicheki naona kidonda kiunoni, si nikapagawa nawaambia watu kwa hamaki, "Oneni nimepigwa risasi", mzee mmoja akasema, "acha ujinga mtoto, risasi ungesimama wewe?". Kumbe vile vioo viliruka vikanichoma aisee. Leo wakati naoga nikayaona haya makovu kiunoni nikaamua niandike hapa.
R.i.p baba Pendo, hakika ilishaandikwa iwe hivyo
Sent using Jamii Forums mobile app