Yusufu R H Sabura
JF-Expert Member
- Jun 26, 2020
- 740
- 828
Habari wanajamvi, Niende moja kwa moja kwenye mada.
Sitaweza kuelezea kwa kina utendaji wake kwa vile Mwenyezimungu bado hajanibariki nafasi hiyo, lakini Nyansaho alikuwa anaogopeka, yaani ni mtu wa kazi kwelikweli.
Nilimfahamu Dr Rhimo Nyansaho mwaka 2020 nilipopata nafasi ya kujitolea na kujifunza kwa vitendo katika benki kongwe ya Azania. Nilikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza pale idara ya sayansi ya siasa mlimani.
wadau wa idara hiyo na baadhi ya wadau wa Coss tower mnafahamu kuwa pale mjengoni mafunzo kwa vitendo ni kwa mwaka wa pili mostly kwa sisi tusiokuwa walimu. Lakini kwa vile napenda mambo makubwa kuliko umri wangu nikasema kukaa likizo tu Hapana wacha nikajitolee, namshukuru Mungu mwaka wa pili nilipata tena nafasi hiyo adimu.
Siku moja asubuhi majira ya saa nne nne hivi nikiwa nafanya shughuli zangu pale ofisini, ghafla uvumi ulianza kutembea mle ndani kwa kasi kuwa boss yu aja ! boss yu aja ! , nilishuhudia wafanyakazi wakijiweka sawa katika nafasi zao, laiti ungeshuhudia walivyokuwa wakijiweka sawa ungesema labda ni wanafunzi wa sekondari wakijiandaa na ugeni wa Mwalimu wa zamu darasani kwao. Mimi mtoto wa field nilipewa tahadhari na senior wangu kuwa makini na kompyuta niache kushangaa namna kiyoyozi kinavyopuliza kwa kasi asubuhi yote ile. Sikuwahi kudhania kwenye maisha yangu ningekuja kufanya kazi benki walau kwa kujifunza tu.
Wakati tunamsubiri Boss awasili ili tuendelee na maisha yetu ya kawaida, mara anaingia binadamu ambaye binafsi nilimuona kama kijana mdogo tu aliyenizidi umri, kwa akili ya haraka haraka nisingeweza kumuita baba au mzee, ningemuita brooo au jombaa !. Mtu huyo alikuwa amevalia Kaunda suti kali ya dark blue Pamoja na miwani, huku akipiga hatua ndefu za taratibu. Mtu yeyote angeona ule mtembeo wa yule mtu angedhani labda ni mkaguzi Fulani hivi. Alitembelea idara zote pale mjengoni na kwa kweli wafanyakazi walionesha kumchangamkia.
Zamu yangu ikafika kijana wa field, Nilimsalima yule mtu lakini sikuwa kwenye great tension yeyote kwa vile nilikuwa bado namsubiri boss anaetajwa kuwa ni boss aingie, kwa vile department yetu ndo ilikuwa ya mwisho basi akageuza akasepa zake.
Senior aliekuwa akinisimamia kazi nlizokuwa napewa akanigeukia akaniambia umemuona huyo jamaa !
Mimi : ndiyo nimemuona
Senior ! : Huyo ndo boss sasa , anaitwa Nyansaho.
Nikapigwa na butwaa, nikasema how can a young man hold such a great position?, Kwenye Qur an kuna mstari unasema Mwenyezimungu humpa amtakaye na kumnyima amtakaye, haya niliyaona kwa Nyansaho, kijana mdogo mwenye majukumu makubwa.
Mara ya pili ujio wa Boss Nyansaho ulitangazwa, hiyo siku nikasema leo sikosei mazee, nikajiweka sawasawa, nikawa makini na desktop ya Azania pale very serious. Boss Nyansaho akafika mbele yangu akanicheeeeki, kimoyomoyo nikasema SEMA KIMEUMANA !, ulikuwa msemo maarufu kwa wakati ule, Boss Nyansaho alitilia shaka umakini wangu na kuhoji ni shughuli gani iliniweka serious kwa kiwango kile cha Daraja la kijazi, aliniuliza kama ni mtoto wa chuo kikuu nikasema ndio ni kweli hujakosea mzee. Basi akiwa anataka kuondoka akatilia maneno kwamba ‘’hawa Watoto wa chuo ni kuwa nao makini sana ! unaweza kuta amekaa serious ukajua anafanya vitu vya maana kumbe anaangalia vyakula vya Kwenda kununua mlimani city, ie chocolates na biskuti’’.
Boss Nyansaho hakujua kwamba kijana anayemuongelea anauwezo wa kufanya kazi yenye kiwango sawa na kile cha bulldozer, naam sijamaanisha hayati JPM Hapana ! bulldozer lile la mzungu, lina rangi ya njano.
Mara ya tatu tena Nyansaho akatinga mjengoni, wakati huo wafanyakazi wametulia zao, hakuna anaejigeuza geuza kwenye vile viti vyao vya kuzungukazunguka kwa sababu mwamba yupo area, Angalau mimi nikajitutumua nikatoka mle ndani, sijui nilikuwa nafuata nini nje lakini ile nafika reception namkuta Nyansaho akienda na kurudi ndani ya chumba hichohicho, alikuwa akitembeatembea huku akiangalia simu yake ya mkononi, ile scene ilinijaza ari zaidi ya kuusaka utawala kwa vyevyote itakavyokuwa bila kujivua utu.
Kwa wale mliofika ile reception ya Obama mtanielewa palivyo pale ndani, wakati Nyansaho akila round za kutosha pale ndani, nikamuona receptionist wa kike mmoja akimsemesha Boss kwa hali zote , siunajua tena ukishakuwa boss , halafu jamaa wala hazingatii wala nini. Kwa sisi vijana tunaojitafuta huwa tunapenda kusemeshwa vile na Watoto wakali lakini hatutoboi sababu hatuna maokoto. Nilimsalimia then nikapita hivi.
Basi ile scene ilinijaza hamu ya kuupania utawala kwa maana muda si mrefu nilikuwa nimetoka kunyanyaswa kimahusiano na mama yenu mdogo, halafu nakuja kushuhudia na kuthibitisha kuwa Madaraka na kina dada ni ndugu ! .
Huyo ndiye Dr Rhimo Nyansaho, ukiacha wanaomuonea wivu juu ya kismart chake cha teuzi jamaa anaheshimika sana, nafikiri kuliko mtu yeyote pale ndani.
Majuzi nilikuwa nazungumza na mkurugenzi wa hazina wa benki ya Azania, I am sorry for mentioning you boss Mwandimila, nafahamu wewe ni boss na mlezi wa kitaasisi kwangu.
Boss Mwandimila aliniambia nikamsalimie Dr Nyansaho, licha ya kunisisitiza nilihisi uoga wa kupandikizwa kulingana na umakini wa mkurugenzi huyo mpya wa PSSSF.
Kwa vile Jamii Forums ni jamvi kubwa Afrika Mashariki, najua Habari hizi zitafika Obama, nitumie fursa hii kutuma salamu Strategy kwa ujumla.
Lakini kwa upekee na kwa nidhamu ya hali ya juu nitume salamu kwa Mkurugenzi wa hazina Mr Gilbert Mwandimila, mzee naomba unifikishie salamu zangu za pongezi kwa Dkt Nyansaho, kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma, nikija tena siku nyingine nitakuomba unipeleke mguu kwa mguu nikamsalimie mana si jambo dogo hilo.
Ombi kwa mheshimiwa Rais : ikiwa andiko hili utalisoma mheshimiwa Rais, likitokea gap lingine, tunakuomba umzingatie na Mkurugenzi wa hazina Mr.Gilbert Mwandimila, kazi anayoifanya pale Obama imetukuka sana.
Asante
rajarajabu99@gmail.com