wamkodowenye
JF-Expert Member
- Aug 26, 2016
- 261
- 290
Inawezekana ukawa na mawazo sana baada ya kupima na ukakutwa na virus vya HIV ila pitia hapa ujifunze kitu binafsi.
Huu ni ushuhuda wangu kwako baada ya mimi kupima na kukutwa na hivi virusi, kiukweli nilijiamini mno hadi yule mpimaji akashangaa ila kiukweli nilikua sijawahi kupima kabisa ila niliwahi kupima baada ya kujua wife ni mjamzito na siku si nyingi ataanza clinic kwahiyo nikaona niwahi.
Nilipokutwa na HIV nilijipa moyo na jinsi ya kuanza kumweleza wife mimi nilijua ndiyo tuu nitakua nimesababisha maana nilikua natoka nje sana kutokana na nature na job yangu. Mke wangu alinichanganya baada ya kumwambia aanze clinic mapema yeye akawa ananiambia hana haraka mpaka afikishe miezi mitano.
Nilikuwa nje ya nchi kikazi niliumia maana sikutaka mtoto azaliwe na maambukizi ya VVU, nilimbembeleza mwishowe nikarudi mapema tukapima tukakutwa wote ni waathirika ilikua ni mziki alipanic sana na akawa anasali akagoma kutumia ARVs.
Nilimbembeleza na kua nae karibu sana akakubali kutumia tukaishi kwa raha zaidi ya mwanzo kajifungua mtoto baada ya miezi mitatu tumempima mtoto ni mzima kabisa kiukweli tunaishi kwa raha na tunaendelea kutumia ARVs na kwa afya tuliyo nayo mtu akikuambia hawa watu wana HIV uwezi amini.
Nimejifunza kitu kimoja kuhusu huu ugonjwa huu ugonjwa haupo mwilini upo akilini mtu akiupata hutanguliza akilini kuwa atakufa hafikirii kua hatoishi milele na huwaza jamii watakutenga ila ukiondoa hii na mkiwa kama mke na mume mkituliza akili mkiishi kama watu wa kawaida mtaishi miaka mingi sana, pia mtalea watoto na kua wakubwa.
Nimeona niweke huu ushuhuda hapa maana najua wapo wengi waoga kupima na wanawaza kupima wakiogopa je akikutwa nao? Pia jifunze kuwa kama upo kwenye ndoa au uchumba unaweza kua mwaminifu bahati mbaya mwenzio akaukuletea pia.