Jinsi limbwata lilivyoleta umasikini katika familia ya mama mwenye nyumba

Amoxlin

JF-Expert Member
May 30, 2016
3,782
4,108
Ndugu wanajamvi poleni na majukumu ya hapa na pale,

Niende moja kwa moja kwenye mada.

Kwa kawaida baadhi ya wanawake hulinda ndoa zao kwa kutumia limbwata ili kuzitawala familia zao hasa kumtawala mme.

Katika utafutaji nilipanga chumba maeneo ya tmk (uwanja wa taifa).
Kabla sijapanga katika nyumba hiyo familia hiyo ilikuwa na maisha mazuri sana na pesa haikuwa tatizo kwa wakati huo (kwa mujibu wa mama mwenye nyumba).

Watoto walipata mahitaji yote ya msingi na vyakula vya kumwaga. Katika harakati za kutaka kumdhibiti mwanaume ili afanye atakayo mke wake, mwanamke aliamua kutafuta dawa (limbwata), alifanikiwa na kuanza kumwekea mmewe katika chakula.

Dawa ilileta mafanikio yaliyovuka mipaka kwani mwanamke aligeuka kuwa kichwa cha familia ila akili na uwezo wa baba wa kutafuta pesa ulipungua kwa kiasi kikubwa sana.

Mzee anawahi kurudi nyumbani kila siku na anatulia ndani bila kutoka, watoto wakikosa haulizi chochote zaidi ya kukaa kimya. Siku zilivyoenda biashara zilianza kufa, kila mtaji uliopatikana ulipotea bila kujua. Mpaka sasa hali ni mbaya sn.

Mzee akitoka kwenda kazini anarudi mikono mitupu, mama akisafiri safari zake hata mwezi mzima au zaidi bila baba kuuliza familia inashinda njaa hivyo wapangaji hujitolea kusaidia watoto.

Matokeo zaidi ya limbwata hilo yamepelekea mama huyo kufanya kazi ngumu ikiwemo kupika vyakula vya kuuzia mashabiki wakati wa mpira pale uwanja wa taifa, kutembeza bidhaa mitaani na zaidi kuwa na michepuko ya kumpatia chochote.

Jamani wadada tuoneeni huruma sie wanaume.
 
Mmmmh!!Hii ni zaidi ya majuto kwa huyo mama,ila wadada achen huu mchezo aisee ni dhambi maana mtu unakuwa sio ww bali kila ufanyalo ni msukumo wa limbwata.
 
Wenye data naomba mnisaidie.

Nimesikia kuna baadhi ya limbwata kuna Wanawake wananyoa nywele sehemu zao za siri, kisha unachanganyiwa kwenye chakula.

Eti ni kweli?
 
Limbwata ni mbaya huua nyota ya mme ila wengi huwa hawalijui hilo coz Mme anakuwa hana uwezo wa kufikiria anakuwa kzezeta kasoro yake t hajinyei na kula kinyesi,
Upo sahihi mkuu.
Nyota ya mwanaume hufifishwa na limbwata na nyota ya mwanamke huwa juu yako xo hata ile akili ya utafutaji nayo hutoweka.
 
safi sana ndo alichokitaka, alichoumba Mungu usitake kuongezea zaidi
Inasikitisha sana, asubuhi watoto wanaomba dawa ya meno kwa wapangaji. Ilinibidi ninunue dawa kubwa maana ilikuwa inaisha haraka sana.
 
Wenye data naomba mnisaidie.

Nimesikia kuna baadhi ya limbwata kuna Wanawake wananyoa nywele sehemu zao za siri, kisha unachanganyiwa kwenye chakula.

Eti ni kweli?
Hapa tungempata mshana jr na mzizi mkavu wangetusaidia.
 
Back
Top Bottom