Jinsi Hospitali ya Mwananyamala ilivyopunguza vifo vya kinamama na watoto wakati wa Uzazi

News Tz1

Member
Joined
Nov 28, 2025
Posts
25
Reaction score
30
56d0f7c5-5309-4358-a3de-1cf64a33d6f5.jpeg
Ni simulizi nzito ambazo wahudumu wa afya hukutana nazo mara chache lakini huziacha alama kubwa moyoni. Wakati mwingine, furaha ya kuzaliwa kwa mtoto hubadilika ghafla kuwa majonzi pale mama anapopoteza maisha wakati wa kujifungua.

Kwa madaktari na wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, hali kama hiyo ndiyo inayowasukuma kufanya kila wawezalo kuhakikisha mama na mtoto wanaondoka salama hospitalini.

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Irene Barongo, anasema kwamba juhudi mbalimbali zilizowekwa zimeanza kuonyesha matokeo chanya katika kupunguza vifo vya uzazi.
b9f3942e-5d70-43c5-ba46-530f93bed3d9.jpeg

Mfano wa picha

Anasema katika mwaka wa fedha 2023/2024 hospitali ilirekodi vifo saba vya kinamama wakati wa uzazi, lakini mwaka uliofuata idadi hiyo imepungua hadi vifo vitatu tu.

“Kuna mambo mengi yamefanyika. Kupitia mpango wa "Mama Samia Sponsorship", madaktari bingwa wengi wamesomeshwa na sasa wanarudi kufanya kazi hospitalini, jambo ambalo limechangia kupunguza vifo vya uzazi kwa kiasi kikubwa,” anasema Dk Barongo.

Kwa mwaka mmoja, Hospitali ya Mwananyamala hupokea kati ya wanawake 5,000 hadi 6,000 wanaojifungua. Kila mama anayefika hospitalini hapo hubeba ndoto ya kupata mtoto wake akiwa salama, na kwa wahudumu wa afya ndoto hiyo huwa wajibu wao wa kila siku.

"Vifo vya watoto wachanga vimepungua"

Mbali na afya ya mama, hospitali hiyo pia imefanikiwa kupunguza vifo vya watoto wachanga. Ambapo Daktari Bingwa wa Watoto, Dk Makena Kato, anasema zamani hospitali hiyo ilikuwa na changamoto kubwa ya vifaa vya kusaidia watoto wenye matatizo ya kupumua mara baada ya kuzaliwa, maarufu kama CPAP (Continuous Positive Airway Pressure).

“Awali tulikuwa na mashine moja tu ya CPAP. Kama mtoto amezaliwa kabla ya wakati au njiti na ana changamoto ya kupumua, ilibidi kusubiri hadi mtoto mwingine amalize kutumia,” anasema Dk.Makena Kato

Anasema hali hiyo iliweka watoto wengi katika hatari kubwa ya kupoteza maisha.

“Fikiria mtoto ana shida ya kupumua halafu hospitali ina mashine moja tu, inakuwa ni kama kupanga foleni. Lakini sasa serikali imeongeza mashine zaidi ya 20, hivyo huduma inapatikana kwa haraka na maisha ya watoto wengi yanaokolewa,” anaeleza

Uhai ni kipaumbele

Hata hivyo, kwa wahudumu wa afya, suala la uhai wa mama linabaki kuwa kipaumbele kikubwa. Dk. Kato anasema kuwa mwanamke ameumbwa kwa namna ya kipekee kuleta uhai duniani, hivyo kupoteza maisha wakati wa kujifungua ni jambo linaloumiza na ambalo linapaswa kuzuilika kadiri iwezekanavyo.

“Ni jambo la kuhuzunisha sana pale mama anapojifungua halafu anafariki. Mungu amemuumba mwanamke kuleta uhai duniani, hivyo kupoteza maisha wakati wa kitendo hicho si haki,” anasema.

Aidha kwa upande wake, Dk Barongo anasema hospitali imeweka mifumo ya haraka ya kujifunza kila pale kifo kinapotokea.

Anasema mara tu tukio la kifo cha mama linapotokea, wahudumu wa afya hukutana ndani ya saa 24 kufanya tathmini ya kina juu tukio hilo.

“Lazima tukutane na kufanya 'mortality review'. Tunajiuliza tumekosea wapi na tunajifunza nini ili jambo hilo lisijirudie tena,” anasema.

Umuhimu wa damu salama

Aidha, anaeleza kuwa hospitali imeimarisha kampeni ya ukusanyaji wa damu salama ili kuhakikisha damu inapatikana wakati wowote inapohitajika kwa wajawazito wenye changamoto wakati wa kujifungua.

“Kampeni kubwa imefanyika katika ukusanyaji wa damu salama. Kwa sasa vifo vingi vinavyotokea havisababishwi na ukosefu wa damu,” anaeleza.
45a7255e-48ef-4cd2-a245-c11112f05062.jpeg

Mfano wa picha

Akizungumzia maadhimisho ya mwezi wa wanawake duniani, Dk Barongo anasema hakuna jambo gumu kwa daktari au muuguzi kama kushuhudia mama akijifungua na kisha kupoteza maisha huku akimuacha mtoto mchanga.

“Cha muhimu ni kuhakikisha hakuna mwanamke anayepoteza maisha wakati wa uzazi. Mama ni kiumbe anayebeba na kuleta uhai duniani, hastahili kufa wakati wa kuleta uhai,” anasema.

Utamaduni uliojengeka sasa, ni kuwa katika wodi za uzazi, kila kilio cha mtoto mchanga ni ishara ya matumaini mapya ya maisha na kwa wahudumu wa afya wa Mwananyamala, kila maisha ya mama yanayookolewa ni ushindi mkubwa wa ubinadamu.
 
View attachment 3557918Ni simulizi nzito ambazo wahudumu wa afya hukutana nazo mara chache lakini huziacha alama kubwa moyoni. Wakati mwingine, furaha ya kuzaliwa kwa mtoto hubadilika ghafla kuwa majonzi pale mama anapopoteza maisha wakati wa kujifungua.

Kwa madaktari na wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, hali kama hiyo ndiyo inayowasukuma kufanya kila wawezalo kuhakikisha mama na mtoto wanaondoka salama hospitalini.

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Irene Barongo, anasema kwamba juhudi mbalimbali zilizowekwa zimeanza kuonyesha matokeo chanya katika kupunguza vifo vya uzazi.
View attachment 3557915
Mfano wa picha

Anasema katika mwaka wa fedha 2023/2024 hospitali ilirekodi vifo saba vya kinamama wakati wa uzazi, lakini mwaka uliofuata idadi hiyo imepungua hadi vifo vitatu tu.

“Kuna mambo mengi yamefanyika. Kupitia mpango wa "Mama Samia Sponsorship", madaktari bingwa wengi wamesomeshwa na sasa wanarudi kufanya kazi hospitalini, jambo ambalo limechangia kupunguza vifo vya uzazi kwa kiasi kikubwa,” anasema Dk Barongo.

Kwa mwaka mmoja, Hospitali ya Mwananyamala hupokea kati ya wanawake 5,000 hadi 6,000 wanaojifungua. Kila mama anayefika hospitalini hapo hubeba ndoto ya kupata mtoto wake akiwa salama, na kwa wahudumu wa afya ndoto hiyo huwa wajibu wao wa kila siku.

"Vifo vya watoto wachanga vimepungua"

Mbali na afya ya mama, hospitali hiyo pia imefanikiwa kupunguza vifo vya watoto wachanga. Ambapo Daktari Bingwa wa Watoto, Dk Makena Kato, anasema zamani hospitali hiyo ilikuwa na changamoto kubwa ya vifaa vya kusaidia watoto wenye matatizo ya kupumua mara baada ya kuzaliwa, maarufu kama CPAP (Continuous Positive Airway Pressure).

“Awali tulikuwa na mashine moja tu ya CPAP. Kama mtoto amezaliwa kabla ya wakati au njiti na ana changamoto ya kupumua, ilibidi kusubiri hadi mtoto mwingine amalize kutumia,” anasema Dk.Makena Kato

Anasema hali hiyo iliweka watoto wengi katika hatari kubwa ya kupoteza maisha.

“Fikiria mtoto ana shida ya kupumua halafu hospitali ina mashine moja tu, inakuwa ni kama kupanga foleni. Lakini sasa serikali imeongeza mashine zaidi ya 20, hivyo huduma inapatikana kwa haraka na maisha ya watoto wengi yanaokolewa,” anaeleza

Uhai ni kipaumbele

Hata hivyo, kwa wahudumu wa afya, suala la uhai wa mama linabaki kuwa kipaumbele kikubwa. Dk. Kato anasema kuwa mwanamke ameumbwa kwa namna ya kipekee kuleta uhai duniani, hivyo kupoteza maisha wakati wa kujifungua ni jambo linaloumiza na ambalo linapaswa kuzuilika kadiri iwezekanavyo.

“Ni jambo la kuhuzunisha sana pale mama anapojifungua halafu anafariki. Mungu amemuumba mwanamke kuleta uhai duniani, hivyo kupoteza maisha wakati wa kitendo hicho si haki,” anasema.

Aidha kwa upande wake, Dk Barongo anasema hospitali imeweka mifumo ya haraka ya kujifunza kila pale kifo kinapotokea.

Anasema mara tu tukio la kifo cha mama linapotokea, wahudumu wa afya hukutana ndani ya saa 24 kufanya tathmini ya kina juu tukio hilo.

“Lazima tukutane na kufanya 'mortality review'. Tunajiuliza tumekosea wapi na tunajifunza nini ili jambo hilo lisijirudie tena,” anasema.

Umuhimu wa damu salama

Aidha, anaeleza kuwa hospitali imeimarisha kampeni ya ukusanyaji wa damu salama ili kuhakikisha damu inapatikana wakati wowote inapohitajika kwa wajawazito wenye changamoto wakati wa kujifungua.

“Kampeni kubwa imefanyika katika ukusanyaji wa damu salama. Kwa sasa vifo vingi vinavyotokea havisababishwi na ukosefu wa damu,” anaeleza.
View attachment 3557917
Mfano wa picha

Akizungumzia maadhimisho ya mwezi wa wanawake duniani, Dk Barongo anasema hakuna jambo gumu kwa daktari au muuguzi kama kushuhudia mama akijifungua na kisha kupoteza maisha huku akimuacha mtoto mchanga.

“Cha muhimu ni kuhakikisha hakuna mwanamke anayepoteza maisha wakati wa uzazi. Mama ni kiumbe anayebeba na kuleta uhai duniani, hastahili kufa wakati wa kuleta uhai,” anasema.

Utamaduni uliojengeka sasa, ni kuwa katika wodi za uzazi, kila kilio cha mtoto mchanga ni ishara ya matumaini mapya ya maisha na kwa wahudumu wa afya wa Mwananyamala, kila maisha ya mama yanayookolewa ni ushindi mkubwa wa ubinadamu.
Afya ni investment sio bla bla.

Good job guys
 
Back
Top Bottom