CCM imezidi kuendeleza
dhulma zake kwa wananchi wa kanda hiyo kwa kuwakosesha soko la uhakika
wa zao za korosho hali iliyopelekea wakulima wa zao hilo kutoa mazao kwa
mkopo kwa wanunuzi,,
utaratibu wa malipo wa stakabadhi ghalani ndio hasa uliokakubaliwa na
kuwapa wakulima tumaini msimu uliopita,,kumbe CCM ilikua inawacheza
shere wakulima hao,na hawakuwa na nia ya dhati katika kuwasaidia,,
Hali ya maisha ya wakulima mkoani humo imezidi kua tete, Jimbo la
Tandahimba Mbunge wa CCM Juma Njwayo ambae amelikimbia jimbo hilo mara
baada ya ushindi wake wa zengwe wa uchaguz wa wizi 2010 dhidi ya
aliyekuwa mgombea wa CUF ndugu Katani,, mbunge huyo kalikimbia jimbo
hilo na wananchi wamempga marufuku kutokanyaga ardhi ile, nyumba yake
ilichomwa moto, mashamba yake yalichomwa moto na gari lake kuvurumishiwa
mawe na wananchi wenye hasira kali kutokana na kukosa kuwajibika na
uzuzu wa mbunge njwayo,,mtwara vijijini jimbo la hawa ghasia hali imekua
hivo hivo,,
Mtwara mjini kuna mbunge hopless sana anaitwa Murji,,yeye kwa
kushirikiana na kaka yake wa damu anaeitwa Abbas,wanatumia kampuni yao
ya ununuzi wa korosho kufanya ulanguzi kwa kununua zao hilo kwa bei sh
600 kwa kilo kutoka 1200 ya msimu uliopita tena kwa mkopo,wamesababisha
hali ngumu kwa wakulima wote wa zao la korosho katika mkoa huo,,
serikali haina usemi kwa kuwa yasemekana JK anapata asilimia fulani
katika mauzo ya zao hilo kwa kampuni hiyo,ikumbukwe JK ndiye aliefanya
uteuzi tata wa Anna Abdallah na Mudhihir Mudhihir kuwa wakuu wa Bodi ya
Korosho jambo lililopeleka kulifanya zao hilo kuwa ni kitega uchumi chao
huku wananchi wakiendelea kunyanyasika na kukosa mwelekeo wa maisha
siku baada ya siku,,
CCM imekosa huruma na WaTz,na ndio maana Kinana na Nape waliambulia
zomea zomea walipodhuru kanda ile, CCM ni sikio la kufa tuiache tuh
ijifie zake na tuikomboe nchi yetu 2015,,
kifo cha CCM 2015 kinawezekana,tuache kulalamika
lalamika,tunaambiana haya sio kwa propaganda kama wanavofanya kina
Nepi,tunaambiana haya yote ili tuzinduke na kila mtu atimize wajibu wake
panapo majaliwa hapo 2015 kwa maslahi ya vizazi vyetu vijavyo,,
jinamizi hili la CCM liishie kizazi hiki hiki,,