Naombeni kufahamishwa endapo kuna dawa au tiba kamili kwa jino nje ya kung'oa.
Ninagalagala sakafuni ile mbaya hino halitulii kabisa awali nilitumia DFP lakini maumivu yamechipuka tena. Ni jino la premolars upande wa juu kushoto, nahisi maumivu makali mpaka mishipa kichwani imenitoka alafu nimevimba vibaya sana, naombeni mnijulishe dawa au tiba halisi au mtaalamu wa meno anisaidie kwa sababu limetoboka na hata nikiswaki hamna damu inayotoka plse msaada ili nikatibiwe maana nateseka balaaa
Asante kwa ushauri mwema bila shaka itanilazimu kuwajibika haraka kuweza kupata suluhu mapema. Labda tu niulize hospitali ipi ina wataalamu wazuri wa meno kwa sababu nakumbuka docta mmoja aliwahi kumng'oa jino rafiki yangu siku hiyo mie ndo nilimpa kampani kwenda basi jamaa akazimia kabisa hali iliyonifanya niogope utoaji wa meno, lakini sasa ndo hivo hamna jinsi
Pole sana mkuu, ingawa nimecheka sana, maumivu ya jino we acha tu!