Jino kwa jino ya Ado Shaibu ni ujinga

Ndata

JF-Expert Member
Mar 2, 2017
226
321
Nimeona Ndugu Ado Katibu Mkuu ACT akidai mwaka huu ni jino kwa jino, kifupi anataka kuturudisha kule tulipotoa Ngali ngali.

Kwanza aina hii ya siasa sio iliyoasisi chama cha ACT, ila kwakuwa wameungana na kundi linaloamini katika siasa za visasi na Chuki huu umekuwa utaratibu wao mpya.

Hofu yangu ni hio jino kwa jino wanamfanyia nani? Wapi na kwa nguvu ipi?

Tunafahamu Kiongozi wa ACT amekuwa na kashfa ya kuuza majimbo akiwa Chadema na hata alipoenda ACT aliendelea na tabia hio. Mfano alikataa Chama kusimamisha mgombea jimbo la Marehemu Filiku Njombe ila alisimamisha kila jimbo linaloongozwa na wapinzani.

Unasema jino kwa jino wakati mliona jinsi Kc alivyokimbia mbio wakati Matiko anakamatwa Tarime. Kweli mnauwezo wa kuyatenda haya mnayoyaongea au ndio mikwara tuu nanyi muonekane mnaongea.

Binafsi sioni maana yoyote ya kauli kama hizi, kwanza ni uongo pili watakaojaa upepo watakuwa disappointed tuu mwisho wa siku.

Mwisho kabisa, hivi bro Ado hio jino kwa jino umeisema kwa kuangalia uimara wa chama chako wapi? Yaani ni wapi nchi hii ACT itaibiwa kura.

Zanzibar mtajigawia kura, ACT, CUF na ADC wakati huku bara jimbo pekee mnalotegemea uhakika wa ushindi ni less than 50%.

 
Naww utakua hivi
FB_IMG_15927496917718688.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom