Jinamizi la soka barani Afrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinamizi la soka barani Afrika

Discussion in 'Sports' started by Kijamani, Nov 20, 2009.

 1. K

  Kijamani Senior Member

  #1
  Nov 20, 2009
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni miezi tu imesalia bara la Afrika litakuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa mnamo mwaka 1936 huko nchini Uruguai.Hakuna utata kwamba mpira wa miguu ndio mchezo wenye mashabiki wengi duniani na kwamba ndio mashindano ambayo hufuatiliwa na idadi kubwa ya watu duniani.
  Miaka yote timu kutoka bara la Afrika zimekuwa zikisindikiza zile za ulaya na zile za amerika ya kusini.Hatua kubwa kufikiwa ni robo fainali ambapo ni sherehe kwa timu husika.Je lini timu kutoka bara hili zitachukua kombe hili?
  Jinamizi hili linaanzia pale ambapo idadi kubwa ya Waafrika wanapokuwa washabiki wa kutupwa wa timu za ulaya hadi inafikia hatua mtu anajiua anapo ona timu yake ya ulaya imefungwa.Cha kushangaza unapowauliza watu kama hawa kwanini wanapenda timu za ulaya kuliko za kwao wanasema hazichezi mpira wa kuvutia.
  Jambo la kujiuliza ni kwamba je ipo siku walikaa na kutafakari kwa nini timu zao hazichezi soka la kuvutia?Na je hizo zinazocheza soka la uvutia zimefanya nini mpaka kufikia hapo zilipo sasa?
  Kwa hakika huu ni utawala wa kifikra ambao tumetawaliwa na wazungu na ndio maana siku zote tutakuwa watazamaji na wasindikizaji wa wazungu.Ipo haja ya sisi kubadilika watu waanze kufikiria mtibwa,Majimaji badala ya asernal.
   
Loading...