Jinamizi la Lowassa latimua wanaCCM 62 Songea

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Wakati CCM Ruvuma ikiwatimua wanachama 62 kwa usaliti ikiwamo kumuunga mkono Edward Lowassa katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, wabunge wa chama hicho wameteua wenzao 15 kufanya tathimini ya uchaguzi huo ikiwamo mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho.

Katika tukio la kwanza, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kupokea maoni kutoka kwa wanachama kupitia vikao kuanzia kata hadi mkoa, na kubaini kuwapo waliokiingiza chama kwenye matatizo makubwa kutokana na usaliti.

Alisema, hadi sasa viongozi tisa wametimuliwa wakiwamo wanachama 53 wa kawaida, baadhi wamepewa onyo kali, wengine walipewa ushauri.

Mwisho alisema mchakato wa kuwawajibisha wengine unaendelea ngazi za juu, kutokana na CCM mkoa kutokuwa na maamuzi nao.

Wabunge wachunguza
Katika hatua nyingine, chama hicho kimeunda kamati maalumu ya wabunge 15 kwenda kutathmini uchaguzi huo badala ya kutegemea ripoti zinazotolewa na makatibu wa wilaya na mikoa pekee.

Hatua hiyo ilifikiwa juzi mjini Dodoma baada ya wabunge wa chama hicho kukutana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana na kukubaliana kuchukua hatua.

Katibu wa wabunge wa CCM, Jason Rweikiza alisema kamati ya wabunge hao itawahoji wabunge wote wa CCM 267 kwa kuwa wao ndiyo wahusika wakuu, kuangalia changamoto walizokutana nazo.

Wajumbe hao 15 ni Joseph Mhagama, Dk Faustine Ndugulile, Joseph Kakunda, Profesa Anna Tibaijuka, Mboni Mhita, Peter Serukamba, Innocent Bashugwa, George Mkuchika, Munira Mustapha, Jasmini Tiisekwa na Abdallah Ulega.

Kamati hiyo itaangalia mfumo wa kura za maoni kwa wagombea ubunge, ili kuondoa watu wasiokitumikia chama ambao wamekuwa wakitumia fedha zao kupitia kwenye kura za maoni.
 
CCM wana kazi sana.

Kimbembe jamaa akikabidhiwa kijiti mwisho wa mwezi huu, mbona watajuta.

Magufuli na CCM yake yaonekana wanaogopa jina Lowassa, kuliko Lowassa mwenyewe.
 
Hakuna mbunge wa ccm ambaye hatumii pesa kuhonga wapiga kura uchaguz mkuu
 
Wacha wafu wazikane
 
CCM wana kazi sana.

Kimbembe jamaa akikabidhiwa kijiti mwisho wa mwezi huu, mbona watajuta.

Magufuli na CCM yake yaonekana wanaogopa jina Lowassa, kuliko Lowassa mwenyewe.
Hivi utulivu huu tunao uona kwa sasa ndani ya ccm ni kwa sababu lowasa ameamua kukaa kimya,ila siku akianza mikutano yake ndio ccm utawasikia wana gawana mbichi
 
CCM wameonyesha hakuna mtu aliye mkubwa kuliko chama. Ndivyo walivyomuondoa Lowassa kwenye mchujo wa urais.
 
Hii safisha safisha itawakuta mpk wabungee ndani ya chama.
Wote watatoka, subiri rais apewe uenyekiti
 
Back
Top Bottom