SeriaJr TW
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 246
- 224
Katika tukio la kwanza, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kupokea maoni kutoka kwa wanachama kupitia vikao kuanzia kata hadi mkoa, na kubaini kuwapo waliokiingiza chama kwenye matatizo makubwa kutokana na usaliti.
Alisema, hadi sasa viongozi tisa wametimuliwa wakiwamo wanachama 53 wa kawaida, baadhi wamepewa onyo kali, wengine walipewa ushauri.
Mwisho alisema mchakato wa kuwawajibisha wengine unaendelea ngazi za juu, kutokana na CCM mkoa kutokuwa na maamuzi nao.
Wabunge wachunguza
Katika hatua nyingine, chama hicho kimeunda kamati maalumu ya wabunge 15 kwenda kutathmini uchaguzi huo badala ya kutegemea ripoti zinazotolewa na makatibu wa wilaya na mikoa pekee.
Hatua hiyo ilifikiwa juzi mjini Dodoma baada ya wabunge wa chama hicho kukutana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana na kukubaliana kuchukua hatua.
Katibu wa wabunge wa CCM, Jason Rweikiza alisema kamati ya wabunge hao itawahoji wabunge wote wa CCM 267 kwa kuwa wao ndiyo wahusika wakuu, kuangalia changamoto walizokutana nazo.
Wajumbe hao 15 ni Joseph Mhagama, Dk Faustine Ndugulile, Joseph Kakunda, Profesa Anna Tibaijuka, Mboni Mhita, Peter Serukamba, Innocent Bashugwa, George Mkuchika, Munira Mustapha, Jasmini Tiisekwa na Abdallah Ulega.
Kamati hiyo itaangalia mfumo wa kura za maoni kwa wagombea ubunge, ili kuondoa watu wasiokitumikia chama ambao wamekuwa wakitumia fedha zao kupitia kwenye kura za maoni.
Source: Mwananchi