Jina la Mdee latumika katika utapeli

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,249
2,000
JINA la Halima Mdee, Mbunge wa Kawe jijini Dar es Salaam linatumiwa na watu matapeli kwa maslahi yao.

Kutokana na hali hiyo, mbunge huyo ameliomba Jeshi la Polisi kudhibiti watu hao ambao wamekuwa wakiwataka wananchi kujiunga na vicoba vilivyopewa jina lake- Halima Mdee Vicoba.

Mdee amesema mataperi hao wamekuwa wakitumia jina lake kuwatapeli watu kwa madai amefungua ofisi ya kutoa mikopo kwa wananchi ambayo ina riba nafuu na mkopo unapatikana ndani ya dakika 45.

“Suala hili limekuwepo kwa muda mrefu nimeishatoa taarifa polisi, mbaya zaidi matapeli hao wanaendelea kuwaibia watu na wanapiga sana fedha kwa kutumia jina langu.

“Naliomba Jeshi la Polisi kupambana na matapeli kwa kuwa, hata namba zao zinajulikana na matapeli hao wanaweza kupatikana,”amesema Mdee.

Ametoa kauli hiyo jana baada ya taarifa ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuzunguka mjini wakiulizia ofisi za Halma Medee Vicoba ili waweze kupatiwa mkopo.

Wanafuzi hao wakizungumza na mtandao huu mjini Dodoma wamesema, wameona matangazo katika mitandao ya kijamii ambayo inaelekeza upatikanaji wa mikopo ya muda mfupi.

Wanafunzi hao wamesema, wamekuwa wakitafuta namna ya kupata fedha za mkopo kwa ajili ya kujiendeleza lakini wamekuwa wakitafuta ofisi zao kama zinavyoelekezwa lakini wameshinda kuzijua.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom