Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,853
Wabunge wa UKAWA watakuja na hoja nyingi za kuibua na kupinga ufisadi Bungeni na kutaka hatua zichukuliwe kwa wahusika na bila shaka wabunge wa CCM na serikali yao watazidiwa kwa hoja na pengine kukosa majibu sahihi.
Kitakachofuta baada ya hali hiyo kujitokeza katika mijadala ndani hiyo Bunge,ni wabunge wa fulani kuja na hoja mbona nyinyi mlimpokea Lowassa na huku mlidai ni fisadi na leo mnajidai kupinga ufisadi n.k.Wanaweza kumtaja moja kwa moja au kwa kumanisha japo hatakuwa na nafasi ya kujitetea kwani hayuko Bungeni jambo ambalo ni kinyume kabisa na kanuni za Bunge.
Niwaambie tu,tuhuma za ufisadi wa Lowassa ni "single" iliyochuja siku nyingi sana kiasi kwamba ni sawa na ..... ya kale ambayo hayuniki tena na single hiyo wala haina mvuto kwa sasa kwani mlishindwa kuimaliza wenyewe ndani ya Bunge na kuamua kufunga mjadal wake.
Single zinazo-hit kwa sasa ni Escrow,uchaguzu wa Zanzibar,bomoaboma,ubaguzi, n.k.ambazo hata mwananchi wa kawaida anaweza hata kuacha shughuli zake na kusikiliza kinachojadiliwa lakini kamwe sio Richomond.Single ya Richmond haiuziki kabisa siku hizi na ushahidi ni kura zaidi ya milioni 6 alizopata mh.Lowassa kwenye uchaguzi mkuu uliopita licha ya yote yaliyosemwa juu yake.
Itakuwa ni kutajana majina mwanzo mwisho kwa wengu watakaopewa nafasi ya kuongea na spika asipokuwa makini,mijadala itavunjika na vijembe kutawala na wanaweza hata kushindwa kufikia maamuzi au kuweka maazimio juu ya hoja za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.
Tusubiri.