PreGE2025 Jimbo la Singida Mjini kuwaniwa na vijana

PreGE2025 Jimbo la Singida Mjini kuwaniwa na vijana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Wakati taifa likielekea katika uchaguzi mkuu na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likitarajiwa kuvunjwa rasmi katika siku chache zijazo, taswira ya kisiasa katika baadhi ya majimbo inabadilika kwa kasi, huku majina mapya yakianza kujitokeza na kuchukua nafasi kubwa kwenye mijadala ya kisiasa.

Moja ya majina yanayotajwa kwa nguvu kubwa katika Jimbo la Singida Mjini ni la Japhari Saidi, kijana mwenye historia ya kujivunia na sifa lukuki zinazomuweka katika nafasi nzuri ya uongozi.

Japhari, mzaliwa wa Kata ya Utemini, ni mtaalamu wa kemia aliyejipatia elimu ya juu ndani na nje ya nchi, akihitimu Shahada ya Sayansi ya Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuendeleza masomo ya uzamili katika Sayansi ya Bioteknolojia na Udhibiti wa Ubora kutoka Chuo Kikuu cha Purdue, Marekani. Kwa zaidi ya miaka 10, Japhari amekuwa mtumishi wa umma katika Wizara ya Afya kupitia TMDA, ambapo amejijengea jina kutokana na weledi, uadilifu, na utendaji wake katika kuhakikisha usalama na ubora wa dawa na vifaa tiba nchini.

Kwa mujibu wa maoni ya wananchi waliotembelewa na Jambo TV, jina la Japhari linatajwa kwa matumaini makubwa hasa kutoka kwa vijana, ambao wanaona ndani yake taswira ya kizazi kipya chenye uwezo wa kuleta mabadiliko chanya. Anaelezwa kuwa ni kiongozi mwenye maono, mchamungu, msikivu kwa watu, na anayeelewa changamoto za jamii za sasa- hasa kwa vijana, wanawake na makundi yenye uhitaji maalum.

“Tunahitaji viongozi wapya, vijana wenye elimu, maadili na dira ya maendeleo. Japhari siyo tu ana sifa hizo, bali pia anaelewa vizuri mfumo wa serikali, jambo linalompa nafasi ya kuanza kutatua matatizo ya wananchi mara moja,” amesema mmoja wa wakazi wa Minga.

Mbali na uzoefu wake kitaalamu, Japhari pia anafahamika kwa ushiriki wake katika shughuli za kijamii, michezo, na harakati za kijamii zinazolenga kuinua maisha ya watu wa hali ya chini. Anaonekana kuwa chaguo la mabadiliko, na tayari kumekuwa na mijadala kuwa iwapo atapata nafasi ya kuwa mbunge, anaweza hata kuteuliwa kushika wadhifa mkubwa zaidi serikalini, kama Naibu Waziri au Waziri kamili, kutokana na sifa zake.
1749801544197.png

source:Jambo online
 
Naona kijana wa utemini anakuja na vision kali sana.

Ajabu wakishapata madaraka wanakengeuka na kuanza kutuita kenge raia tulio wapa dhamana ya kuwa hapo. ,
 
Back
Top Bottom