Giddy Mangi
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 830
- 184
Siha kila kijiji kina maji,na sasa vimebaki vijiji nane tu ambavyo havina umeme,barabara za siha zimetanda vijiji vyote! Najua unataka Ubunge jenga hoja tu kwa wananchi ila mkoa wa kilimanjaro hakuna jimbo ambalo limefanikiwa kwa maendeleo kama Siha Mwanri amefanya kazi sana! Wewe wambie wananchi mabadiliko ya kupata mbunge mwingine ni mhimu kwenye barabara,maji,umeme usiguse watakushangaa na kukuona uko nyuma ya wakati!
umetaja maji hujagusia Afya ambapo katika mkoa wa Kilimanjaro ni Wilaya ya Siha hawana hospitali ya wilaya wala ya Shirika lisili la kiserekali inayoweza kufanya kazi kama hospitali teule ya Wilaya..... kikubwa hawana Ambulance, gari la kubeba wagonjwa nashindwa kuelewa mbunge wao kama Waziri TAMISEMI kashindwa kusaidia hapa... wanafikisha ngonjwa late hospitali za KCMC, Mawenzi. ukipata ndugu anahitaji rufaa toka Siha kwenda KCMC ama Mawenzi ndo utajua nazungumza nini hapa. U simtetee bado hajafanya kazi huyu mbunge.
Mjadala mzuri sana huu. Ni wa maendeleo badala ya siasa na porojo. Tungekuwa na mingi ya namna hii ya kuwapa changamoto wabunge na viongozi wengine. Hongereni akina Mangi. Kama kawaida.Unachekesha sasa Hospitality ya Kibong'oto iko wapi? Tena ni hospital Bingwa ya Kifua Kikuu ipo SIHA na inatoa na huduma mbalimbali ukiacha Kifua kikuu! Siha inaenda kwa kasi sana ilinganishe na Hai utaona hai wapo palepale!
Unachekesha sasa Hospitality ya Kibong'oto iko wapi? Tena ni hospital Bingwa ya Kifua Kikuu ipo SIHA na inatoa na huduma mbalimbali ukiacha Kifua kikuu! Siha inaenda kwa kasi sana ilinganishe na Hai utaona hai wapo palepale!
Siha kila kijiji kina maji,na sasa vimebaki vijiji nane tu ambavyo havina umeme,barabara za siha zimetanda vijiji vyote! Najua unataka Ubunge jenga hoja tu kwa wananchi ila mkoa wa kilimanjaro hakuna jimbo ambalo limefanikiwa kwa maendeleo kama Siha Mwanri amefanya kazi sana! Wewe wambie wananchi mabadiliko ya kupata mbunge mwingine ni mhimu kwenye barabara,maji,umeme usiguse watakushangaa na kukuona uko nyuma ya wakati!
Holy crap.Jimbo la Siha lina changamoto nyingi ikiwemo Miundombinu,Afya,Elimu na uwajibikaji wa watendaji wa Serikali.Mbunge wa Siha Mh.Agrey Mwandri amekuwa Mbunge kwa miaka Kumi sasa na japo kuwa kofia ya pili ndani ya serikali ya Ccm tena wizara nyeti ya TAMISEMI ameshindwa kufanya mambo ya msingi na pia ameshidwa kutatua kero za wana wa Siha kwani kero kubwa zikiwemo Elimu,Afya,Miundombinu ya barabara na Masoko bora bado ni kero zinazo wakabili watoto,baba,mama,bibi na babu zake Mh Mwandri ambaye anasikifa sana kwa majibu mazuri ndani ya Bunge hili hali akiwa amewasahau wapiga kura wake tena ambao uwakumbuka tuu wakiwa na misiba na pia wakati wa kampeni akiwafuata kwenye vilabu vya mbege na kuwanunulia ikiwa ni njia ya kuomba kura.NAOMBA MSAADA WA MAWAZO TUWASAIDIE VIPI WANA SIHA.
Be blessed... Nirejee kwenye mada: Ukiachilia kelele zake na usanii aliojaliwa, hamna cha ajabu ndani ya miaka kumi ya UBUNGE wa Mwanri. Wanywa gongo, wazururaji, na aina hiyo wameongezeka mno sambamba na umasikini unaokua kila leo. Sustainable development efforts ndio kitu nataka sikia. Tell me about that!
barabara ya Lawate Kashashi hadi Forest imechakachuliwa na serikali imetenga tema M.30 ambazo zimeanza kuliwa na ushahidi upo.
Jaman tusilete ushabiki wa kisiasa usiokuwa na tija katika jimbo letu la siha nani asiyejua aliyo yafanya Mwanri tangu atupiwe mzigo na Makidara???????Ndugu Giddy mangi, naona umekuja na propaganda kali.
Swali:: Ilikuwaje mpaka jimbo la Siha likawa Wilaya?? Unajua ilivyokuwa vigumu kuaccomplish hilo jambo??
Sasa baada ya kuwa Wilaya, unataka ASAP kuwe na Hospitali ya Wilaya wakati KCMC ni karibu??
Suala la Umeme vipi Siha?? Je maji salama vipi na huo mradi mkubwa wa Wajerumani?? Barabara za Lami mpaka huko Sanya Juu vipi?? Shule za Sekondari kila kona nazo vipi??
Wilaya bado inachangamoto nyingi ambazo zinaendelea kushughulikiwa. The fact kuwa SIHA ni Wilaya imeleta benefits nyingi mno na zingine zitaendelea kuonekana jinsi siku zinavyokwenda.
Kwa hiyo Mwanri kuwa Waziri Tamisemi ulitaka afanye ufisadi na kupendelea SIHA kwa gharama ya kutekeleza wilaya zingine nchini?? Huyu mtu sio wa dhuluma na anafanya kazi kwa manufaa ya nchi wakati huo huo akijaribu kuleta maendeleo Siha kwa juhudi bila kucompromise wilaya nyingine maskini ndani ya TAnzania.
Jaman tusilete ushabiki wa kisiasa usiokuwa na tija katika jimbo letu la siha nani asiyejua aliyo yafanya Mwanri tangu atupiwe mzigo na Makidara???????
Ni msiha gani asiyefahamu ilivyokuwa shughuli pevu wasiha kujikomboa mikononi mwa wamachame??kama hujui kaulizie hilo tu linatupa pa kuanzia kwa wasiha wote kwa ujumla!!!!1
Mtu anasema wanasiha wamemchagua mwanri kwa kuwanywesha gongo au mbege ndani ya siha kuna wasomi wazuri tu unataka kuniambia wote hawa wamedanganywa na gongo au mbege?