fredy mziray
New Member
- Sep 20, 2012
- 4
- 0
Wanazuoni na wasomi mbalimbali toka katika vyuo vikuu nchini wakishirikiana na makada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na wananchi wote wataelekeza nguvu zao zote kulikomboa jimbo hili ambalo ni sawa na halina mbunge kwa sasa kutoka katika ukoloni mpya wa chama cha mapinduzi. Tunasikitika sana kuona wananchi wakiteseka kwa shida ya maji na miundombinu mibovu. Pia tunastaajabu kuona halmashauri ikifumbia macho ujenzi mbovu wa barabara ya lami inayoelekea katika hifadhi ya taifa ya mkomazi ambayo imekuwa na viraka kabla hata ya kufikisha miaka mitano. Ni vyema CCM ikaanza kufungasha virago mapema kuliko kukutana na aibu itakayowakuta baada ya kupoteza jimbo hilo.