Unaweza ukawa na degree hata 12 kichwani lakini zikawa hazina maana yoyote kwa jamii inayokuzunguka.Ndugu FESTUS LIMBU kipindi anagombea ubunge kwa mara ya kwanza pale jimboni MAGU watu walikuwa na matumaini makubwa sana kwake mpaka wakampa na ukamanda wa jimbo hilo kipindi MASHISHANGA ni mkuu wa mkoa wa MWANZA.Lakini leo hii mheshimiwa kalitegea kisogo jimbo na hataki hata kwenda kusikiliza kero zao.Binafsi nahisi ameamua kulitoa sadaka hilo jimbo kwa CHADEMA.Kwa ufupi Limbu hataki kusikia kitu CCM Pale MAGU.
Jimbo ameshalikabizisha kwa members wa CHADEMA ndo wanaofanya kazi kama jimbo liko chini yao.