Jimbo jipya la uchaguzi 2020.

Jimbo jipya la uchaguzi 2020.

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2015
Posts
4,649
Reaction score
5,074
Amani kwenu wadau wa JF.
Kufuatia watanzania wengi kukumbwa na majanga yaliyoletwa na serikali pamoja na kushindwa kuwasaidia wananchi hao hasa hili la vyeti feki

Ninakusudia kuanzisha sehemu maalumu ambayo tutaishi kama jamaa moja na kuwa na sauti moja.

Naamini kwa wingi wa wahanga hawa pamoja na ndugu zao,tutatosha
kuunda jimbo la uchaguzi na wilaya.

Kama una ndugu,rafiki,jirani tafadhari mjulishe kusudio hili na umpe matumaini mapya ya kuwa na maisha ya furaha.

Wengine tutawaruhusu pia,kama watakuwa na mlengo sawa na wetu.

MIMI NDIYE NITAKUWA MBUNGE WENU KWA AWAMU MOJA TU 20…25,NIWE SAUTI YENU KATIKA HILO JIMBO JPYA. Ninaahidi kutowaangusha katika uwakilishi huo.

Nafasi nyingine za uteuzi wa rais,nitamshauri naye kutekeleza jukumu hilo kadiri ya katiba yetu.

Hivyo mtie shime jamaa yako anaweza kupata ukuu katika hilo jimbo la waliojumbwa na misukosuko.

Litakuwa jimbo/wilaya la mfano hapa tanzania. Maisha bora yatakuwa hapo.

Upembuzi yakinifu wa sehemu bado unaendelea,ikiwa ni pamoja na kupata vibali rasmi vya kuanzisha makazi. Utakapo kamilika tu,mtajulishwa tuanze kufika.
Tanzania, Hima himaaaaa.
 
Back
Top Bottom