Jiji larindima! Mnyika afunika!

mi bado sielewi iweje hawa wabunge wengine washinde kesi zao mahakamani isipokua LEMA... hivi yule hakimu pale arusha hajisikii vibaya kuona mahakimu wenzake wamefanya demokrasia na haki isipokua yeye
 
safi sana..hawa jamaa walisoma upepo wakaona ya LEMA yasije yakajirudia mikoa ya pwani yoote ikageuka NGOME YA CHADEMA...ila moto wa petrokl ushawashwa kwenye nyasi kavu...

So its too late... it's so bad!
 
Watu wana mapenzi mabaya hivi Jiji la Dar es Salaam linaweza kurindima sababu ya Mnyika, kwanza kuna watu wengine hata huyo Mnyika hawamajui.

hahaaaaaaa mchuzi wa bata bwana umenifurahisha
 
Watakuambia Dar ni ya ukanda wa kaskazini
Ni kweli, Ubungo na Kawe wamejazana watu wenye hulka na tabia za Kaskazini. Majimbo ya Segerea mtalichukua pia, dalili zipo wazi na Ukonga kuna kina mura wengi, nao hawatupendi. Ila majimbo ya Kusini mwa Dar (Kigamboni na Temeke, Magamba tunapetaaaa..!, chezea watu wa Kusini weye? Jimbo la Ilala, magwanda labda mtegemee kura za Kitunda, ila humu mujini Wahindi na Wazaramo wa Kariakoo, Magomeni, Jangwani tumewaweka mfukoni, hamtuwezi.
 

Acha ubishi usio na maana wewe, nunua mwanananchi la leo lina habari kamili ya maanadamano na jinsi POLICCM walivyojitahidi kumuomba Mh. apande gari lakini wananchi wenye mwamko wa mabadiliko walikataa wakawa hawana namna zaidi ya wao pia kujiunga kwenye maanadamano hadi kimara zilipo ofisi za mbunge.
 
pwani ya bagamoyo nayo inabidilika labda Tabora

Tabora inasikitisha wakuu wangu, acha mambo mengine yaani hata bendera za CDM tu zinahesabika, kama sio 5 basi 6 mji mzima, ila sio mbaya tumeanzia Igunga, Nzega na tutatawanya kote Tabora
 

hii yaelekea ilikuwa siku ya kutangazwa kuwa mbunge kwa uelewa wako.
 

Attachments

  • juu-mnyika.jpg
    20.7 KB · Views: 44
usiseme hatujasikia mirindimo ya furaha, sema sijasikia' na kwakua haijakufurahisha habari ya ushindi wa mnyika, wewe ni miongoni mwa wale wachache ambao daima wanapingana na ukweli wa maisha.
 
usiseme hatujasikia mirindimo ya furaha, sema sijasikia' na kwakua haijakufurahisha habari ya ushindi wa mnyika, wewe ni miongoni mwa wale wachache ambao daima wanapingana na ukweli wa maisha.

Well said mdau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…