Jiji la Dar, lazindua mfumo wa Kidigitali wa kufuatilia Miradi ya maendeleo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,931
12,216
Wakuu,

Jiji la Dar, limezindua mfumo utakaowezesha kufuatilia Miradi yote inayoendelea Mkoa wa Dar.

Mfumo huu Utaongeza Usimamizi, Uwajibikaji na upokeaji taarifa kwa haraka na mapema zaidi.

Akizindua mfumo huo, Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda, amesema imefika wakati Taasisi zote na mikoa yote kuwa na kifumo ya Kidigitali kwani dunia ya sasa imebadilika, wenzetu wapo kwenye speed ya internet ya 5G sisi huku bado tunafanyankazi kizamani.

Ametolea mfano, Leseni zote za biashara inatakiwa zisajiliwe kidigitali kuliko kuwekeza kwenye magari ya kufuatilia leseni Mitaani. Mtu leseni inakaribia kueisha muda wake anatumiwa meseji ya taarifa kama ilivyo kwenye Ving'amuzi.

Makonda amedai kwamba kuna Watendaji wanatoa taarifa zisizo sahihi kuhusu Viwanda. Anadai kuna viwanda kumbe vilishajifia. Hivyo kaagiza wana IT kuandaa mfumo wa Kidigitali wa kutambua Viwanda Vyote vilivyopo Dar na mtaa Kiwanda kilipo.

Kawataka watu wa matangazo nao wahamie Digitali.

Kahimiza watendaji wote wafundishwe jinsi ya kutumia mfumo kuanzia ngazi ya chini. Sasa hakuna haja ya kufuatana maofisini, ukifanya kazi unajaza kwenye mfumo ikiambatana na picha.
 
Nimemwelea sana aliposema kuna watendaji wanatoa taarifa za uongo kuhusu viwanda hapo angeanza kuhoji wanasema ndani ya miaka nne kuna viwanda elfu 4 vimejengwa je viko wap?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…