Jiji la Arusha lapeta huduma bora

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Halmashauri ya Jiji la Arusha imeendelea kuwa Jiji lenye kutekeleza miradi na huduma bora kwa wananchi wake nchini.

Leo nimeongoza jopo la wataalum wa Jiji mbele ya kamati ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa (LAAC) juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na maagizo ya kamati na mapendekezo ya mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali za halmashauri ya Jiji la Arusha 2015/2016.

Kamati imeridhika na utendaji wa Jiji na mwaka ujao watatembelea Jiji la Arusha kujionea kwa vitendo.Pongezi kwa wah madiwani ,wataalam na watendaji wote na wananchi kwa kuendelea kutuunga mkono.Umoja wetu Nguvu yetu.
 
Halmashauri ya Jiji la Arusha imeendelea kuwa Jiji lenye kutekeleza miradi na huduma bora kwa wananchi wake nchini.Leo nimeongoza jopo la wataalum wa Jiji mbele ya kamati ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa (LAAC) juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na maagizo ya kamati na mapendekezo ya mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali za halmashauri ya Jiji la Arusha 2015/2016.Kamati imeridhika na utendaji wa Jiji na mwaka ujao watatembelea Jiji la Arusha kujionea kwa vitendo.Pongezi kwa wah madiwani ,wataalam na watendaji wote na wananchi kwa kuendelea kutuunga mkono.Umoja wetu Nguvu yetu.
dacf564a15c4a41287965dfb017162ca.jpg
7815d44a5118a0d587c12c2eba575bf3.jpg
8678bb03d1994499781e093c80115e00.jpg
 
Kuchora ramani ya Tanzania ni sawa na kuoga, lazima uanzie kichwani.
 
Hongereni jiji dogo la Arusha lenye muonekano mzuri baada ya jiji la Rock city___hongereni sana.
 
Hongereeni sana, lakini msiendelee kununua madiwani. Mkibaki masisemu tupu kwenye mjengo maendeleo hakuna.
 
Jitahidini kuirejesha mji wa Arusha ktk hali yake ya awali ktk kuhakikisha mnatenga maeneo mahususi kwa wafanyabiashara. Ndani ya miaka miwili iliopita hadi sasa maeneo yasio rasmi kwa biashara ndogo ndogo yamekuwa kero kwa watumiaji wengine wa barabara hasa maeneo ya Idara ya Maji kuelekea Stand kuu ya mabasi ya mikoani. Eneo lingine ni pale Friends corner kwenye taa za kuongozea magari nikero tupu hasa jioni. Sijawahi kuona nyanya karoti na vitunguu vikiuzwa katkati ya mji wakati kuna maeneo maalum kwa biashara hizo.

Rai yangu kwenu nawaombeni rejesheni Mji wa Arusha ktk hali yake ya awali.
 
Back
Top Bottom