JIipu nyumbani kwa Magufuli wilaya ya Chato

karasinga

Member
Oct 2, 2011
7
0
Habari za kazi mimi ni mwananchi ninaeishi katika kijiji cha MUSASA kata ya makurugusi wilaya ya Chato mkoa wa Geita.

Malamiko yangu ni kwamba hapa kijiji cha Musasa kumegeuka mgodi wa Dhahabu wa wachimbaji wadogo tatizo langu sio mgodi wa dhahabu tatizo ni wizi wa mapato ya serikali ya kijiji na serikali kuu na dhuruma wanayofanyiwa wachimbaji wadogowadogo na wafanyabiashara hapa kijijini .

Kwa ulewa wangu mapato yote yanatakiwa yakusanywe na yasimamiwe na serikali lakini sio kinachotendeka hapa kijijini kwetu.

Kuna watu wamejitokeza ndio wanakusanya mapato yote ikiwa ni ushuru wa biashara, ushuru wa wachimbaji wadogo,ushuru wa mrahaba wa madini. Kwa taarifa tulizo nazo mkurugenzi wa CHATO alipeleka vitabu vya risiti kwa ajiri ya ukusanyaji ushuru kwa serikali ya kijiji na ghafla baada ya kukabidhi vitabu siku ya pili alitoa tamko kwa serikali ya kijiji warudishe vitabu vya serikali vya kukusanyia ushuru (HW5) vyote na kuacha kikundi cha watu wanaojiita ni wakala wa madini(TUJIKOMBOE ) kukusanya ushuru bila stakabadhi za serikali.

Hii Tujikomboe inasimamiwa na diwani wa CCM wa Buserere anaejulikana kwa jina la Godfrey Miti na diwani wa Makurugusi Alex Kagisa.

Inasemakana DC wa wilaya ya CHATO anashindwa kulinda na kutetea maslahi ya kijiji na serikali na sisi wachimbaji wadogo kwakuwa kuna mtu wa juu toka wizarani anazuiwa kutekeleza majukumu.

Tunaomba suala hili lifutiliwe kwa makini kwakuwa kijiji kinapoteza mapato yake na serikali kwakuwa shughuri za kijamii na biashara zinafanyika hapa kijijini.

Na sasa toka wasitishe ukusanyaji wa mapato ya serikali ni mwezi umepita.
 

Attachments

  • IMG-20160209-WA0003.jpg
    IMG-20160209-WA0003.jpg
    46.4 KB · Views: 65
  • IMG-20160209-WA0005.jpg
    IMG-20160209-WA0005.jpg
    64.5 KB · Views: 72
  • IMG-20160209-WA0006.jpg
    IMG-20160209-WA0006.jpg
    29 KB · Views: 60
  • IMG-20160209-WA0007.jpg
    IMG-20160209-WA0007.jpg
    29 KB · Views: 37
  • IMG-20160209-WA0008.jpg
    IMG-20160209-WA0008.jpg
    34.4 KB · Views: 50
  • IMG-20160209-WA0009.jpg
    IMG-20160209-WA0009.jpg
    34.4 KB · Views: 54
Back
Top Bottom